KISWAHILI DARASA LA 4
SURA YA KWANZA.
UMAHIRI WA LUGHA
Katika sura hii utasoma habari kuhusu mahafali ya darasa Ia saba. Kutokana na habari hiyo utaweza kujifunza kuhusu maneno yenye maana za jumla. Pia, utajifunza maneno ya kundi moja na kuweza kuyatumia katika sentensi.
Ufahamu
Soma habari ifuatayo kisha jibu maswali.
Mahafali ya darasa Ia saba
Leo ni siku ya mahafali ya dada yangu Tunu. Amehitimu darasa la saba katika Shule ya Msingi Mtibwa. Jana mwalimu alitutangazia tuwahi shuleni kufanya usafi kabla wageni hawajafika.
Tulifika shuleni saa 12:30 asubuhi na tuligawana kazi kwa madarasa. Wanafunzi wa darasa Ia kwanza na la pili waliokota takataka eneo lute la shule. Wanafunzi wa darasa la tatu na la nne tulifagia madarasa na kupiga deki. Wanafunzi wa darasa la tano na la sita walikusanya kuni na kuchota maji. Wanafunzi wa darasa Ia saba hawakupangiwa kazi.
Wapishi waliandaa vyakula mbalimbali kwa ajili ya mahafali. Walipika pilau, wali, ndizi, nyama, njegere na maharage. Pia, walipika mboga za majani ambazo ni mchicha, kisamvu na majani ya kunde. Vilevile, waliandaa matunda kama mananasi, maembe na machungwa.
Jukwaa kubwa liliandaliwa kwa ajili ya wageni watakaokaa katika meta kuu. Pembeni mwa jukwaa hilo, kulikuwa na maturubai yaliyofungwa kwa ajili ya kivuli. Sehemu hiyo ilikuwa ni maalumu kwa wazazi na wageni waalikwa. Maeneo yote ya shule yalipambwa kwa maputo ya rangi ya bluu, kijani na nyekundu.
Ilipofika saa 3:00 asubuhi wazazi na wageni waalikwa walianza kuwasili. Tuliwakaribisha na kuwapeleka sehemu iliyoandaliwa kwa ajili yao. Wahitimu nao walikuwa tayari wameketi sehemu yao wakiwa wamevaa sare za shule.
Baada ya nusu saa Mgeni Rasmi aliwasili. Mwenyekiti wa kamati ya shule, mwalimu mkuu na wajumbe wa kamati ya shule walimpokea Mgeni Rasmi. Waliongozana naye hadi meza kuu. Wakati huo wote sisi sate tulisimama, tukipiga makofi, nderemo na vifijo vilisikika huku tukiimba wimbo ufuatao:
Karibuni wageni wetu, karibuni wageni x 2 Karibuni shule ya Mtibwa, karibuni wageni x2 Sisi ni nani jama, sisi wanafunzi x2
Taifa linatutegemea, wazazi wanatutegemea, Sisi wanafunzi.
Tuliimba wimbo huo hadi wageni walipokaa kwenye viti. Mshereheshaji alimkaribisha Mwalimu Mkuu kwa ajili ya kuwakaribisha na kuwatambulisha wageni. Baada ya utambulisho, vikundi mbalimbali vya burudani vilitumbuiza.Kulikuwa na nyimbo, maigizo, mashairi na ngonjera. Wageni waalikwa pamoja na wahitimu walifurahi sana.
Ilipofika saa 6:30 adhuhuri,Mgeni Rasmi alipewa nafasi ya kutoa nasaha kwa wahitimu. Aliwatahadharisha kuepukana na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI. Baada ya hapo alitoa zawadi. Zawadi zilitolewa kwa wahitimu waliofanya vizuri katika masomo, nidhamu, uongozi na michezo. Hatimaye aliwakabidhi wahitimu vyeti kisha akapiga picha pamoja nao.
Ilipofika saa 7:30 mchana, wageni pamoja na wahitimu walikwenda kupata chakula. Wanafunzi wengine tulikwenda kupata chakula katika madarasa yetu. Ilipofika saa 9:30 alasiriwageni waliondoka na wanafunzi tuliruhusiwa kurudi nyumbani.
ZOEZI LA KWANZA.
UFAHAMU.
- Katika shule ya mtibwa kulikua na tukio gani?
- Kkazi gani walifanya wanafunzi shuleni?
- Kwanini wanafunzi wa darasa la saba hawakupangiwa kazi?
- Wapishi walipika nini?
- Mgeni rasm aliwaasa nini wahitimu?
- Umejifunza nini kutokana na habari ulioisoma?
ZOEZI LA PILI
Tunga sentensi ukitumia maneno yafuatayo;
- Mahafali
- Alfajiri
- Wasili
- Alasiri
- Adhuhuri
- Hitimu
- Mshereheshaji
- Kutuimbuiza
ZOEZI LA TATU
MAZOEZI YA LUGHA.
A. Andika sentensi hizi kwa lugha sanifu na hati nadhifu
- Mkono yangu ilichafuka nikaosha
- Motto yake ana miguu mbili
- Kitabu hii nzuri ni ya nani?
- Chakula yangu ilikua tamu
- Mpira ndogo imeanguka
- Maji ilimwagika yote
- Nyumba letu ni nzuri
- Kuku hizi ni za mjomba yangu
- Maembe mangu mameiva
- Kifuli cha mlango ule kimepotea.
B. Andika maneno manne yanayowakilishwa na neon la jumla namba (i) ni mfano.
Na. |
Neno la jumla |
Maneno |
1 |
Nguo |
Sketi, kaptura, shati, fulana |
2 |
Rangi |
|
3 |
Mboga |
|
4 |
Wanyama |
|
5 |
Vinywaji |
|
6 |
Mchezo |
|
7 |
Matunda |
|
8 |
Mikoa |
|
9 |
Wadudu |
|
10 |
Chakula |
C. Pigia mstari neon lililo tofauti na maneno mengine katika kundi.
- Sufuria, bakuli, kikombe, viatu
- Nyumba, gari, pikipiki, baiskeli
- Shati, suruali, taa, gauni
- Ali, juma, kunguru, maria
- Macho, pua, mboga, mdomo
- Karoti, hoho, vitunguu, chupa.
- Baba, mama, ndama, mjomba
D. Andika na ukamilishe methali hizi kwa kimalizio sahii
- Pole pole ndio………………………………
- Njia ya mwongo ni……………………………
- Teke la kuku halimuumizi………………………..
- Harahaka haina……………………………………………
- Mtaka yoye hukosa………………………………
- Adui……………………………………………….
- Kawia…………………………………………
- Umoja ni………………………………………..
- Kuuliza si…………………………………………..
- Bendera hufuata………………………………….
E. Andika kwa wingi.
- Jina limeandikwa
- Swali litaulizwa
- Godoro linapendeza
- Goti linauma
- Dawati limefungwa
- Jiko linawaka
- Jino litaota
- Kufulu limeanguka
- Gurudumu limetoboka
- Jani linapendeza
F. Jibu maswali haya kwa ufasaha.
- Mtoto wa mwanagu nitamwita…………………………………
- Kitukuu ni mtoto wa……………………………………………..
- Dada anamtoto anayeitwa Rukia, mimi nitamwita Rukia…………………..
- Mama mdogo ambaye ambaye ni mke wa baba nitamwita…………………….
- Baba wa mama yangu ni………………………………..
- Kaka ya baba yangu ni……………………………………….
- Dada wa baba yangu ni………………………………………
- Mtoto wa mjomba utamwita………………………………………….
- Mama wa nyanya yangu ni………………………………………
- Sauda ni mtoto wa kike wa mama, kwa hivyo nitamwita……………
G. Kanusha sentensi zifuatazo
- Sisi tunakula nyama ya ng’ombe
- Mama hupika chakula na mboga za majani
- Sufuria, bakuri, na vijiko hupatikana darasani
- Samaki ni chakula chenye wanga
- Mbwa anakula majani
- Popo hutaga mayai
nukuu.elimufix.com
SURA YA KWANZA
KUTAJA NENO MOJA LINALOBEBA MAANA YA JUMLA
Katika sura hii utasoma habari kuhusu mahafali ya darasa la saba. Kutokana na habari hiyo utaweza kujifunza kuhusu maneno yenye maana za jumla. Pia, utajifunza maneno ya kundi moja na kuweza kuyatumia katika sentensi.
Ufahamu
Soma habari ifuatayo kisha jibu maswali.
Mahafali ya darasa Ia saba
Leo ni siku ya mahafali ya dada yangu Tunu. Amehitimu darasa Ia saba katika Shule ya Msingi Mtibwa. Jana mwalimu alitutangazia tuwahi shuleni kufanya usafi kabla wageni hawajafika.
Tulifika shuleni saa 12:30 asubuhi na tuligawana kazi kwa madarasa. Wanafunzi wa darasa la kwanza na Ia pili waliokota takataka eneo lute la shule. Wanafunzi wa darasa Ia tatu na la nne tulifagia madarasa na kupiga deki. Wanafunzi wa darasa Ia tano na la sita walikusanya kuni na kuchota maji. Wanafu-= wa darasa Ia saba hawakupangiwa kazi.
Wapishi waliandaa vyakula mbalimbali kwa ajili ya mahafali. Walipika pilau, wall, ndizi, nyama, njegere na maharage. Pia, walipika mboga za majani ambazo ni mchicha, kisamvu na majani ya kunde. Vilevile, waliandaa matunda kama mananasi, maembe na machungwa.
Jukwaa kubwa liliandaliwa kwa ajili ya wageni watakaokaa katika meza kuu. Pembeni mwa Jukwaa hilo, kulikuwa na maturubai yaliyofungwa kwa ajili ya kivuli. Sehemu hiyo ilikuwa ni maalumu kwa wazazi na wageni waalikwa. Maeneo yote ya shule yalipambwa kwa maputo ya rangi ya bluu, kijani na nyekundu.
Ilipofika saa 3:00 asubuhi wazazi na wageni waalikwa walianza kuwasili. Tuliwakaribisha na kuwapeleka sehemu iliyoandaliwa kwa ajili yao. Wahitimu nao walikuwa tayari wameketi sehemu yao wakiwa wamevaa sare za shule.
Baada ya nusu saa Mgeni Rasmi aliwasili. Mwenyekiti wa kamati ya shule, mwalimu mkuu na wajumbe wa kamati ya shule walimpokea Mgeni Rasmi. Waliongozana naye hadi meza kuu. Wakati huo wote sisi sote tulisimama, tukipiga makofi, nderemo na vifijo vilisikika huku tukiimba wimbo ufuatao:
Karibuni wageni wetu, karibuni wageni x 2 Karibuni shule ya Mtibwa, karibuni wageni x2 Sisi ni nani fama, sisi wanafunzi x2
Taifa linatutegemea, wazazi wanatutegmea, Sisi wanafunzi.
Tuliimba wimbo huo hadi wageni walipokaa kwenye viti. Mshereheshaji alimkaribisha Mwalimu Mkuu kwa ajili ya kuwakaribisha na kuwatambulisha wageni. Baada ya utambulisho, vikundi mbalimbali vya burudani vilitumbuiza. Kulikuwa na nyimbo, maigizo, mashairi na ngonjera. Wageni waalikwa pamoja na wahitimu walifurahi sang.
Ilipofika saa 6:30 adhuhuri, Mgeni Rasmi alipewa nafasi ya kutoa nasaha kwa wahitimu. Aliwatahadharisha kuepukana na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI. Baada ya hapo alitoa zawadi. Zawadi zilitolewa kwa wahitimu waliofanya vizuri katika masomo, nidhamu, uongozi na michezo. Hatimaye aliwakabidhi wahitimu vyeti kisha akapiga picha pamoja nao.
Ilipofika saa 7:30 mchana, wageni pamoja na wahitimu walikwenda kupata chakula. Wanafunzi wengine tulikwenda kupata chakula katika madarasa yetu. Ilipofika saa 9:30 alasiri wageni waliondoka na wanafunzi tuliruhusiwa kurudi nyumbani.
1. Katika shule ya Mtibwa kulikuwa na tukio gani? Kazi gani walizifanya wanafunzi shuleni?
E. Cheza na wenzako mchezo ufuatao:
Simameni katika umbo Ia duara huku mkiwa mmeshikana mikono. Kisha kiongozi ataje maneno yaliyokolezwa rangi na ninyi mtajibu alichokisema kiongozi. Kiongozi atataja majina ya vitu mbalimbali vilivyo,kolezwa rangi. Endapo kilichosemwa ni sahihi mruke na kuitikia kwa kutaja jina la jumla Ia kitu alichokitaja. Kama si sahihi msiruke, mkae kimya. Atakayekosea atoke nje ya mduara. Mmoja atakayebaki mpaka mwisho ndiye mshindi.
Mnyama mnyama mnyama - mnyama
Ng'ombe mnyama
Mbuzi - mnyama
Gari (kimya)
Kondoo - mnyama
Tunda tunda tunda - tunda
Nanasi - tunda
Kijiko - (kimya)
Parachichi - tunda
Chungwa - tunda
Mti mti mti mti
Mfenesi - mti
Waridi - (kimya)
Mchungwa - mti
Mchongoma - mti
Ndege ndege ndege ndege
Kuku - ndege
Bata - ndege
Popo - (kimya)
Kasuku - ndege
Samaki samaki samaki - samaki
Sato - samaki
Kambare - samaki
Nyoka - (kimya)
Kibua - samaki
(ii) Taja majina ya jumla yaliyotajwa katika mchezo uliocheza.
- Simulia sherehe uliyowahi kuhudhuria.
- Andika habari uliyoisimulia kWa kuzingatia mwongozo ufuatao.
- Kichwa cha habari.
- Nani walishiriki katika sherehe hiyo?
- Kitu gani kilifanyika kabla ya sherehe?
- Mambo gani yalifanyika wakati wa sherehe?
- Kitu gani kilikufurahisha katika sherehe hiyo?
Ufahamu
Soma na wenzako kisha muigize majigambo yafuatayo:
Tunda: Mimi ni tunda, tukiwa wengi tunaitwa matunda.
Matunda hayo yanaweza kuwa maembe, ndizi, mananasi au mapapai. Kazi yetu ni kuwapatia binadamu vitamin'. Binadamu akitumia matunda atajikinga na maradhi. Pia, ataongeza damu mwilini. Nani kama tunda?
Mti: Mimi ni mti, tukiwa wengi tunaitwa miti. Kuna miti
ya miembe, michungwa, mipera au miarobaini. Miti ina faida nyingi sang. Miti huzuia mmomonyoko wa udongo. Baadhi ya miti hutoa matunda. Majani, mizizi pamoja na magome ya miti hutumiwa na binadamu kutengeneza dawa. Miti hutoa hewa ya oksijeni na huleta mvua. Nani kama mti?
Mnyama: Mimi ni mnyama, tukiwa wengi tunaitwa wanyama. Kuna ng'ombe, mbuzi au kondoo. Huwapatia binadamu kitoweo, mbolea pamoja na maziwa. Ngozi yangu hutumika kutengenezea mikoba, viatu pamoja na mikanda. Nyama yangu husafirishwa nje ya nchi, hivyo husaidia kuinua uchumi wa nchi. Nani kama mnyama?
Mdudu: Mimi ni mdudu, tukiwa wengi tunaitwa wadudu.
Tunaweza kuwa nyuki, nzi, mbu, panzi, siafu, mende, nge au buibui. Miongoni mwetu wengine ni hatari na wengine si hatari. Tunamsaidia binadamu kupata majibu ya vitendawili vyake. Kama huamini tegua vitendawili vifuatavyo:
- Ana miguu ya msumeno.......................
-
Anang'ata kwa mkia.........................
Nani kama mdudu?
Zoezi la Ufahamu
Katika majigambo uliyosoma, kati ya tunda, mti, mnyama na mdudu unapenda kuwa nani? Kwa nini?
- Eleza faida nyingine za miti ambazo hazikutajwa katika majigambo uliyosoma.
- Katika majigambo uliyosoma mdudu anasema, "Miongoni mwetu wengine ni hatari na wengine si hatari." Taja wadudu ambao ni hatari na wasio hatari kwa binadamu.
Kanusha sentensi zifuatazo:
Mfano: Watoto wanacheza ngoma. Watoto hawachezi ngoma.
- Sisi tunakula nyama ya ng'ombe.
- Mama hupika chakula na mboga za majani.
- Sufuria, bakuli na vijiko hupatikana darasani.
- Samaki ni chakula chenye wanga.
- Mbwa anakula majani.
- Popo hutaga mayai.
Andika majigambo kwa kutumia vyombo viwili vya usafiri.
Mfano: Baiskeli: Mimi ni baiskeli.
Ni usafiri rahisi na wenye gharama nafuu.
Kila mtu anaweza kuninunua. Nani kama baiskeli?
Zoezi
Tunga sentensi kwa kutumia maneno yafuatayo:
- Mahafali
- Alfajiri
- Wasili
- Alasiri
- Adhuhuri
- Hitimu
- Mshereheshaji
- Kutumbuiza
Andika maneno manne yanayowakilishwa na neno la jumla. Namba tis ani mfano.
Namba |
Neno la jumla |
Maneno |
nguo |
Sketi, kaptura, shati, fulana |
|
Rangi |
||
Mboga |
||
Wanyama |
||
Vinywaji |
||
Michezo |
||
Matunda |
||
Mikoa |
||
Wadudu |
||
Chakula |
Pigia mstari neno lililo tofauti na maneno mengine katika kikundi
Mfano: kanga, mwewe, kalamu, njiwa .
- Sufuria, bakuli, kikombe, viatu.
- Nyumba, gari, pikipiki, baiskeli.
- Shati, suruali, taa, gauni.
- Ali, Juma, kunguru, Maria.
- Macho, pua, mboga, mdomo.
- Karoti, hoho, vitunguu, chupa.
- Baba, mama, ndama, mjomba.
Kanusha sentensi zifuatazo:
Mfano: Watoto wanacheza ngoma.
Watoto hawachezi ngoma.
- Sisi tunakula nyama ya ng’ombe.
- Mama hupika chakula na mboga za majani.
- Sufuria, bakuli na vijiko hupatikana darasani.
- Samaki ni chakula chenye wanga.
- Mbwa anakula majani.
- Popo hutaga mayai.
nukuu.elimufix.com