NOTES ZA SAYANSI DARASA LA TANO 2026
Mtaala Mpya wa Mwaka 2026
MADA ZA SAYANSI DARASA LA 5 MTAALA MPYA
Sura ya Kwanza: Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula
Dhana ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula
Sehemu za mfumo wa mmeng'enyo wa chakula
Kasoro katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula
Tabia sahihi za ulaji wa chakula
Sura ya Pili: Ukuaji katika mimea na wanyama
Dhana ya ukuaji katika mimea na wanyama
Ukuaji katika mimea
Mahitaji muhimu katika ukuaji wa mimea
Ukuaji katika wanyama
Hatua za ukuaji katika mwili wa binadamu
Njia za kuhimili mabadiliko yanayotokea wakati wa balehe
Sura ya Tatu: Mfumo wa uzazi
Dhana ya mfumo wa uzazi wa binadamu
Mfumo wa uzazi wa binadamu
Kasoro katika mfumo wa uzazi
Utunzaji wa mfumo wa uzazi
Sura ya Nne: Usumaku
Dhana ya usumaku...
Maumbo ya sumaku
Sifa za sumaku
Matumizi ya sumaku
Utunzaji wa sumaku
Msamiati
Sura ya Tano: Usimbaji katika kompyuta
Muundo wa kudhibiti mlolongo
Vibadilika na opereta
Muundo wa kudhibiti maamuzi
Kuchora maumbo kwenye Scratch
SURA YA KWANZA: MFUMO WA MMENG’ENYO WA
CHAKULA
Dhana ya mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
Mmeng'enyo wa chakula ni mchakato wa kibaiolojia ambapo
chakula huvunjwavunjwa kuwa chembechembe ndogo zenye virutubisho ambavyo mwili unaweza
kufyonza. Virutubisho hivi hutumiwa na mwili kwa ajili ya kupata nishati,
ukuaji, matengenezo ya tishu zilizoharibika na ulinzi wa mwili dhidi ya
magonjwa. Ili mwili uweze kupata virutubisho hivi, chakula lazima
kivunjwevunjwe kuwa chembechembe ndogo zinazoweza kufyonzwa na kutumiwa na
mwili. Mmeng'enyo wa chakula hufanyika katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.
Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ni mkusanyiko wa ogani au
viungo vya mwili wa binadamu vinavyohusika na kuvunjavunja chakula kuwa chembechembe
ndogo zenye virutubisho zinazoweza kufyonzwa na kutumiwa na mwili. Ili
kudumisha afya ya mfumo huu, ni muhimu kula mlo kamili kwa wakati sahihi,
kunywa maji ya kutosha, kuepuka kula vyakula vyenye mafuta au sukari kwa wingi
ili kuimarisha afya ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. Mbali na binadamu,
wanyama wengine pia wana mifumo ya kumeng'enyachakula inayotofautiana kutokana
na aina ya vyakula wanavyokula.
Sehemu za mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula unahusisha ogani mbalimbali
ambazo hufanya kazi kwa pamoja ili kurahisisha uvunjwaji wa chakula. Mfumo wa
mmeng'enyo wa chakula wa binadamu huanzia kwenye kinywa hadi kwenye njia ya
haja kubwa. Mfumo huu unajumuisha njia ya chakula, ogani na tezi zinazofanya
kazi pamoja. Sehemu kuu za njia ya chakula ni kinywa, koromeo, umio, mfuko wa
tumbo, utumbo mwembamba, na utumbo mpana kama inavyoonekana kwenye Kielelezo.
Utumbo mwembamba unajumuisha duodeni na iliamu. Vilevile, utumbo mpana
unajumuisha koloni, puru na njia ya kutolea haja kubwa. Ogani zinazounda mfumo
wa mmeng'enyo wa chakula ni pamoja na ulimi, ini, kongosho, na kibofu nyongo.
Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula pia unajumuisha tezi za mate na zile
zinazopatikana katika mfuko wa tumbo. Vilevile, baadhi ya ogani kama ini,
kongosho na kibofu nyongo zina tezi zinazozalishavimeng'enya vinavyotumika
katika kumeng'enya chakula.
Kielelezo: mfumo wa mmeng’enyo wa chakula wa
binadamu
Kinywa
Mchakato wa mmeng'enyo wa chakula huanzia kinywani, ambako
chakula hutafunwa na kuvunjwavunjwa na meno. Pia, katika sehemu hii, vyakula huchanganywa
na mate. Vyakula vyenye wanga huanza kumeng'enywa katika sehemu hii na kisha
kusafirishwa kupitia umio hadi mfuko wa tumbo.
Koromeo
Ni sehemu ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula inayopatikana
kati ya kinywa na umio. Kazi yake ni kuongoza chakula kutoka kinywani hadi kwenye
umio. Chakula huzuiwa kuingia kwenye njia ya hewa kwa kutumia kifuniko
kinachofunga njia ya hewa wakati wa kumeza chakula. Kifuniko hicho huitwa
kidakatonge.
Umio
Umio ni bomba lenye misuli linalounganisha koromeo na sehemu
ya juu ya mfuko wa tumbo. Chakula husafiri kupitia umio kutokana na mfululizo wa
ukazaji na ulegezaji wa misuli ya kuta za umio. Hali hiyo huifanya misuli ya
kuta za umio kusukuma chakula kuingia katika mfuko wa tumbo.
Mfuko wa tumbo
Ndani ya mfuko wa tumbo, chakula huchakatwa zaidi kwkaosa msaada
wa asidi na vimeng'enya. Asidi na vimeng'enya hivi husaidia kumeng'enya protini,
wanga na mafuta, na kubadilisha chakula kuwa mchanganyiko mzito unaoitwa chime.
Kisha, mchanganyiko huo husafirishwa Kwenda kwenye utumbo mdogo ili
kumeng'enywa zaidi na kuruhusu ufyonzwaji wa virutubisho.
Utumbo mwembamba
Sehemu hii inapatikana kati ya mfuko wa tumbo na utumbo
mpana. Sehemu ya mwanzo ya utumbo mwembamba huitwa duodeni. Duodeni hupokea
vimeng'enya kutoka kwenye kongosho na nyongo kutoka kwenye kibofu nyongo kwa
ajili ya kuvunjavunja chakula. Mmeng'enyo wa chakula vyenye wanga, protini na
mafuta hufanyika katika sehemu hii. Sehemu ya mwisho ya utumbo mwembamba huitwa
iliamu. Mchakato wa mmeng'enyo wa vyakula vyenye wanga huishia katika iliamu. Chakula
kinapofika kwenye iliamu, kinachochea ukuta wa iliamu kutoa majimaji. Majimaji
haya yana vimeng'enya ambavyo huendelea kumalizia mmeng'enyo wa protini, wanga
na mafuta. Kazi ya utumbo mwembamba ni kufyonza virutubisho kutoka kwenye
chakula kilichomeng'enywa ili viweze kutumika katika kazi mbalimbali mwilini.
Utumbo mpana
Utumbo mpana unapatikana baada ya utumbo mwembamba. Kazi yake
ni kufyonza maji na madini kutoka kwenye mabaki ya chakula na kuyarejesha mwilini.
Pia, kutumia mabaki ya chakula kutengeneza kinyesi kwa ajili ya kutolewa nje ya
mwili. Vilevile, utumbo mpana una bakteria wenye manufaa wanaosaidia
kumeng'enya mabaki ya chakula na kutengeneza baadhi ya vitamini. Koloni, puru
na njia ya kutolea haja kubwa ni sehemu za utumbo mpana.
Koloni
Sehemu ya kwanza ya utumbo mpana inaitwa koloni. Sehemu hii
hutumika kurejesha maji mwilini kutoka kwenye chakula kilichovunjwavunjwa. Pia,
ni mahali ambapo baadhi ya virutubisho kama vitamini hutengenezwa na bakteria
wanaopatikana katika sehemu hii. Koloni hutumika pia katika kuhifadhi kinyesi
kabla ya kutolewa nje ya mwili.
Puru
Ni sehemu ya pili ya utumbo mpana ambapo kinyesi huhifadhiwa
kwa muda kabla ya kutolewa nje ya mwili kama haja kubwa. Sehemu hii hudhibiti
uondoaji wa kinyesi kutoka mwilini.
Njia ya kutolea haja kubwa
Hii ni sehemu ya mwisho ya utumbo mpana ambayo hutumika
kutolea kinyesi. Kinyesi hutolewa nje ya mwili kupitia njia ya kutolea haja
kubwa.
Kinyesi ni mabaki ya chakula ambayo hayakumeng'enywa na
kufyonzwa na mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.
Kasoro katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula unaweza kuathiriwa na kasoro
mbalimbali zinazoweza kupunguza ufanisi wa uvunjaji-vunjaji wa chakula au
ufyonywaji wa virutubisho. Kasoro katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ni hali
inayoathiri utendaji kazi wa kawaida wa mfumo wa mmeng'enyo wa chakula na
kufanya iwe vigumu kwa mwili kumudu kumeng'enya na kufyonza chakula ipasavyo.
Kasoro hizo zinaweza kuwa za kimaumbile, kurithi au zinazotokana na mtindo wa
maisha na lishe duni. Baadhi ya kasoro za mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ni
kama zifuatazo:
Kupata choo kigumu
Hii ni kasoro katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula
inayosababisha ugumu wa kupitisha kinyesi au kuwa na kinyesi kigumu na kikavu.
Kasoro hii husababishwa na ulaji wa vyakula vyenye kiwango cha chini cha
nyuzinyuzi, kutokunywa maji ya kutosha na ukosefu wa mazoezi ya mwili. Pia,
matatizo ya kiafya kama vile utendaji duni wa utumbo mpana husababisha kupata
choo kigumu.
Njia za kuzuia
Hali hii huzuiawa kwa kula vyakula vyenye nyuzinyuzi za
kutosha kama vile matunda na mbogamboga, kunywa maji ya kutosha na kufanya
mazoezi mara kwa mara.
Kuvimbiwa
Ni hali ambayo mfuko wa tumbo hujaa, kuwa mgumu au kuvimba,
mara nyingi hutokana na mkusanyiko wa gesi katika mfuko wa tumbo. Tatizo la kuvimbiwa
husababishwa na kula chakula kingi kupita kiasi, kula vyakula vinavyosababisha
gesi au tumbo kutovumilia baadhi ya vyakula. Dalili za mtu aliyevimbiwa ni
kuumwa tumbo, kuhisi tumbo kujaa gesi na kupiga mbweu. Wakati mwingine gesi
hiyo huwa na harufu kali na mbaya.
Njia za kuzuia
Ili kuzuia kuvimbiwa unapaswa kula chakula kwa kiasi na
kutafuna polepole ili kupunguza kiasi cha hewa inayomezwa. Vilevile, kunywa maji
ya kutosha ili kurahisisha mmeng'enyo wa chakula katika mfuko wa tumbo.
Kupunguza ulaji wa vyakula vyenye gesi kama vile maharagwe na unyweji wa
vinywaji vyenye gesi kama vile soda. Pia, ulaji wa matunda na mboga za majani
huzuia kuvimbiwa.
Kiungulia
Hii ni hali inayojitokeza wakati asidi kutoka kwenye mfuko wa
tumbo inapopanda hadi kwenye umio na kusababisha maumivu au muwasho katika koo.
Dalili za kiungulia ni pamoja na kuhisi maumivu ya kuungua kifuani. Pia,
kucheua sana na kuhisi uchachu mdomoni. Kiungulia husababishwa na kula chakula
kingi kupita kiasi. Pia, husababishwa na kula vyakula vyenye viungo vingi au
vyenye mafuta mengi. Vyakula hivi huchukua muda mrefu zaidi kumeng'enywa na
vinaweza kuongeza uzalishaji wa asidi tumboni. Sababu nyingine ya kiungulia ni
kula vyakula vyenye asidi kama limau na ndimu kwa wingi. Vinywaji kama vile
soda, kahawa na pombe vinaweza kusababisha kiungulia. Pia, kula chakula muda
mfupi kabla ya kwenda kulala kunaweza kusababisha kiungulia.
Njia za kuzuia
Unaweza kuzuia kiungulia kwa kula chakula taratibu ili
kurahisisha mmeng'enyo wa chakula. Pia, kula chakula kidogokidogo lakini mara kwa
mara. Njia nyingine ni kupunguza ulaji wa vyakula vinavyosababisha kiungulia
kama vile chungwa, limao, chenza, viazi, maharagwe na nyanya. Pia, viungo na
mafuta mengi ni miongoni mwa vyakula vinavyotakiwa kuepukwa. Epuka kulala mara
tu baada ya kumaliza kula. Vilevile, epuka kufanya mazoezi au kazi ngumu muda
mfupi baada ya kula chakula. Hali ya kiungulia ikizidi ni vyema kupata ushauri
wa kitabibu.
Vidonda vya tumbo
Hali hii hutokana na kuchubuka kwa utando wa ute kwenye ukuta
wa mfuko wa tumbo. Michubuko hiyo husababishwa na ulaji wa vyakula vyenye asidi
na kukaa na njaa kwa muda mrefu. Pia, maambukizi ya bakteria husababisha
michubuko katika kuta za mfuko wa tumbo. Asidi iliyoko kwenye mfuko wa tumbo
huunguza kuta zenye michubuko na kutengeneza vidonda. Vidonda vya tumbo huleta
maumivu makali tumboni. Mara nyingi vidonda vya tumbo vikiwa vikubwa huvuja
damu. Dalili za vidonda vya tumbo ni pamoja na maumivu makali kama ya kuungua
kwenye mfuko wa tumbo. Dalili nyingine ni kutapika damu na kupata haja kubwa
iliyochanganyika na damu.
Njia za kuzuia
Unaweza kuepuka vidonda vya tumbo kwa kula kwa wakati na
kupunguza
ulaji wa vyakula vyenye asidi nyingi. Vilevile, kuacha kuvuta
sigara,
kunywa pombe au vinywaji vikali husaidia kuzuia vidonda vya
tumbo.
Tabia sahihi za ulaji wa chakula
Tabia sahihi za ulaji wa chakula ni muhimu ili kudumisha afya
bora na kuzuia matatizo yanayoweza kujitokeza katika mfumo wa mmeng'enyo wa
chakula. Ulaji sahihi unajumuisha mlo kamili wenye makundi yote ya vyakula kwa
uwiano unaofaa. Makundi haya ya vyakula hujumuisha wanga, protini, mafuta,
vitamini, madini na maji. Pia, ni muhimu kuwa na muda maalumu wa kula na
kupunguza kukaa muda mrefu bila kula au kula vyakula visivyo na virutubisho vya
msingi. Tunashauriwa kula vyakula vya nafaka zisizokobolewa na kunywa maji ya
kutosha ili kuuwezesha mfumo wa mmeng'enyo wa chakula kufanya kazi kwa ufanisi.
Ni vema kunywa maji nusu saa kabla au baada ya kula ili kuboresha mfumo wa mmeng'enyo
wa chakula. Ukizingatia tabia hizi, utaboresha afya ya mwili na kujikinga dhidi
ya matatizo kwenye mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.
SURA YA PILI: UKUAJI KATIKA MIMEA NA
WANYAMA
Dhana ya ukuaji katika mime ana Wanyama
Ukuaji katika mimea na wanyama ni mchakato unaojumuisha
kuongezeka au kubadilika kwa ukubwa wa maumbile, yaani urefu, upana, pamoja na uzito.
Ukuaji ni mabadiliko ya kudumu usioweza kubadilishwa. Mabadiliko haya, hutokea
kutokana na kurefuka na kuongezeka kwa idadi za seli na mgawanyiko wa seli
katika kufanya kazi fulani. Mimea hukua kwa kuongeza urefu wa ncha za mizizi na
shina. Pia, mmea hukua kwa kuongezeka kwa mzingo wa shina. Vivyo hivyo, wanyama
hukua kwa kuongezeka kwa urefu na uzito wa miili yao.
Ukuaji wa mimea na wanyama hupitia hatua mbalimbali za
mabadiliko. Kwa mimea, mabadiliko yanahusisha kuota kwa mbegu, kutokea kwa majani,
mizizi na sehemu nyingine kama vile maua, na mbegu au matunda.
Kwa upande wa wanyama, mabadiliko hujumuisha mabadiliko ya
umbo la mwili na tabia. Mfano wa mabadiliko kwa wanyama ni buu kubadilika na
kuwa kipepeo na mtoto kukua na kuwa mtu mzima. Mabadiliko katika mimea na
wanyama yanahusisha mabadiliko ya kimwili na kitabia ambayo ni muhimu kwa
maisha ya mmea au mnyama.
Ukuaji katika mimea
Hatua za ukuaji wa mmea ni mfululizo wa mabadiliko
yanayotokea katika vipindi mbalimbali vya maisha ya mmea kuanzia kuota kwa
mbegu hadi kufa kwake. Kila hatua ina mabadiliko yanayosaidia mmea kukua na
kuendelea na mzunguko wa maisha yake. Hatua hizo ni kuota kwa mbegu, hatua ya
mche, ukuaji wa majani, hatua ya uzazi na hatua ya uzee.
Kielelezo: hatua za ukuaji wa mmea
(a) Hatua ya kuota kwa mbegu
Mbegu iliyokomaa huanza kuota pale inapopata mahitaji muhimu
ya uotaji ambayo ni mwanga wa jua, maji, hewa, virutubisho na jotoridi
linalostahili. Katika hatua hii, mizizi huanza kutoka katika kitungamizizi
kilichopo kwenye mbegu na kukua kuelekea kwenye udongo. Mizizi hufyonza maji na
virutubisho kutoka katika udongo ili kusaidia uotaji. Pia, shina chipukizi huanza
kuota kutoka katika kiinishina kilichopo kwenye mbegu na kukua kuelekea juu ya
udongo ili kuanza kutengeneza shina na majani. Katika hatua hii chakula
kilichohifadhiwa katika mbegu hutumika ili kuipa mbegu nguvu ya kuota.
(b) Hatua ya mche
Baada ya kuota kwa mbegu, hatua ya mche hufuata. Katika hatua
hii, mche huanza kukua kwa haraka. Idadi ya majani huongezeka, mizizi huendelea
kukua na kuimarika ndani ya udongo ili kufyonza maji na virutubisho. Katika
hatua hii kiwango cha chakula huwa kidogo, hivyo mche huanza kutengeneza
chakula chake chenyewe kupitia usanisinuru.
(c) Hatua ya ukuaji wa majani
Katika hatua hii, mmea huendelea kukua na idadi ya majani
huongezeka. Mizizi, shina na matawi huendelea kukua na kuimarika. Mmea
huendelea kujitengenezea chakula chake kupitia usanisinuru.
(d) Hatua ya uzazi
Hii ni hatua ambayo mmea hukomaa na kubadilika kutoka katika
hatua ya ukuaji wa majani hadi hatua ya uzazi. Katika hatua hii, baadhi ya mimea
huanza kuotesha machapuo. Machapuo haya huendelea kukua na kuwa maua ambayo
yana sehemu za uzazi. Maua huchavushwa na kurutubishwa na kupelekea kuwa
matunda au mbegu. Matunda yana mbegu ambazo hutumika kuzalisha mimea mipya.
Mimea kama tikitimaji, chungwa, nyanya, parachichi, mahindi, na maharagwe
huzalisha matunda yenye mbegu. Hata hivyo, kuna baadhi ya mimea ambayo haitoi
maua, lakini huzalisha mbegu zinazoweza kuota na kutengeneza mimea mipya.
(e) Hatua ya uzee
Uzee ni mchakato wa asili wa kuzeeka kwa mimea, ambapo
mgawanyiko wa seli katika kufanya kazi fulani hukoma. Hii husababisha tishu na
ogani za mmea kupoteza uwezo wake wa kufanya kazi polepole hadi kufikia hatua
ya kufa. Hatua hii hutokea katika hatua zote za ukuaji wa mmea japokuwa kasi
yake huongezeka kwa baadhi ya mimea baada ya kutoa mbegu. Tofauti na mimea ya
msimu mmoja, mimea ya muda mrefu uzee hutokea katika ogani kama vile majani na
maua. Hii huiruhusu mimea hiyo kuendelea kuishi na kukua kwa miaka mingi hata
baada ya ogani hizo kufa na kuondolewa.
Mahitaji muhimu katika ukuaji wa mimea
Mimea hukua na kustawi vizuri pale inapopata mahitaji yake
muhimu.
Kielelezo: mahitaji muhimu katika ukuaji wa
mmea.
Ukuaji wa mmea hutegemea upatikanaji wa mahitaji muhimu
ambayo ni mwanga wa jua, hewa, maji, virutubisho na jotoridi stahiki ili
kuiwezesha kukua vizuri. Ukosefu wa moja ya mahitaji haya huweza kuathiri
ukuaji wa mmea. Kwa mfano, mmea unaweza kupata mwanga wa jua wa kutosha, lakini
ukikosa maji au virutubisho vya kutosha, ukuaji huathirika. Yafuatayo ni
mahitaji muhimu kwa ukuaji wa mimea:
Mwanga wa jua
Mwanga wa jua husaidia mimea kukua vizuri. Jua hutoa nishati
ya mwanga na joto. Mimea hutumia nishati ya mwanga kujitengenezea chakula
chake. Majani ya mimea yana umbijani ambalo husharabu mwanga wa jua ili kusaidia
kutengeneza chakula cha mmea. Mchakato wa mimea kutumia mwanga wa jua, maji na
kabonidayoksaidi kutengeneza chakula chake huitwa Usanisinuru. Bila mwanga wa
jua wa kutosha, mimea haiwezi kukua vizuri kwa sababu itakosa chakula.
Hewa
Mimea hutumia gesi ya kabonidayoksaidi katika usanisinuru.
Gesi hii huchukuliwa na mimea kupitia matundu yaliyopo kwenye majani yanayoitwa
stomata. Stomata hufunguka na kuruhusu gesi ya kabonidayoksaidi kuingia ili
kuiwezesha usanisinuru kukamilika. Upungufu wa gesi ya kabonidayoksadi
husababisha kupu mimea kujitengenezea chakula chake. Mimea inahitaji oksijeni
ambayo hutumika kuunguza chakula na kutengeneza nishati inayohitajika ukuaji wa
mimea.
Maji
Maji ni mojawapo kati ya mahitaji muhimu katika ukuaji wa
mimea. Mimea huhitaji maji ili iweze kukua vizuri. Vilevile, maji ni mojawapo
ya mahitaji muhimu katika usanisinuru. Maji hufyonzwa kutoka kwenye udongo kupitia
mizizi. Ncha za mizizi zina vinyweleo vidogo ambavyo husharabu maji kwa njia ya
osimosisi. Baada ya maji kufyonzwa huingia katika mzizi, kisha husafirishwa
kupitia shina hadi kwenye majani. Umuhimu wa maji katika ukuaji wa mimea ni:
(a) Kuyeyusha virutubisho kwenye udongo ili viweze kufyonzwa
na mizizi. Virutubisho husaidia mimea kukua vizuri.
(b) Kusafirisha chakula na kusambaza kutoka kwenye majani Kwenda
sehemu zingine za mimea.
(c) Kusawazisha kiwango cha joto katika mimea.
(d) Kufanya mimea kuwa imara.
(e) Kusaidia mimea kujitengenezea chakula chake kupitia
usanisinuru.
Virutubisho
Mimea inahitaji aina mbalimbali za virutubisho kama vile
madini na vitamini ili iweze kukua vizuri. Virutubisho vya msingi kwa ukuaji wa
mmea ni pamoja na naitrojeni, fosiforasi na potasiamu. Virutubisho hivi
hufyonzwa na mimea kutoka ardhini kupitia mizizi. Mimea hupata virutubisho
kutoka kwenye udongo au sehemu nyingine ilipopandwa. Vinyweleo vidogo vilivyopo
kwenye ncha za mizizi hufyonza maji na virutubisho kwa njia ya osimosisi. Baada
ya kuingia kwenye vinyweleo vya mizizi, virutubisho husafirishwa kupitia mzizi
mkuu hadi kwenye shina na hatimaye kufikishwa sehemu mbalimbali za mmea.
Jotoridi
Mimea huhitaji jotoridi sahihi ili iweze kukua vizuri.
Jotoridi sahihi ni muhimu wakati wa uotaji wa mbegu na usanisinuru. Jotoridi
likiwa juu kupita kiasi, mimea hupoteza maji na kukauka. Pia, jotoridi la chini
hufanya mimea kushindwa kusanisi chakula chake, mbegu kushindwa kuota na hata kupelekea
mimea kufa.
UKUAJI KATIKA WANYAMA
Ukuaji wa wanyama hutegemea uwepo wa mahitaji muhimu kama
hali ya hewa na mazingira yanayofaa, lishe bora na upatikanaji wa maji ya
kutosha.
Lishe bora
Wanyama wanahitaji mlo kamili unaojumuisha virutubisho vyote
muhimu kama protini, wanga, mafuta, vitamini na madini. Upungufu wa virutubisho
hivi katika chakula unaweza kusababisha ukuaji hafifu na maendeleo duni ya
mwili.
Hali ya hewa na mazingira
Wanyama huathiriwa na mazingira wanamoishi. Hali zisizofaa
kama joto kali, baridi kupita kiasi, hewa isiyo safi, na uhaba wa nafasi huweza
kusababisha msongo wa mawazo na kupunguza kasi ya ukuaji wao. Ili miili ya
wanyama ifanye kazi kwa ufanisi, wanahitaji joto la wastani. Aidha, kiwango
sahihi cha mwanga katika mazingira kinahitajika katika ukuaji wa wanyama. Kwa
baadhi ya spishi, mwanga wa kutosha huchochea hamu ya kula na uzalishaji wa
homoni, hivyo kuongeza kasi ya ukuaji na uzalishaji.
Maji
Wanyama wanahitaji maji safi na salama katika ukuaji wao.
Maji ni hitaji muhimu katika shughuli za mwili kama mmeng'enyo wa chakula,
udhibiti wa joto la mwili na usafirishaji wa virutubisho ndani ya mwili.mambo
haya yote ni muhimu kwa ukuaji wa wanyama. Ifuatayo ni mifano ya mabadiliko
mbalimbali katika ukuaji wa wanyama:
(a) Vipepeo hupitia hatua mbalimbali za ukuaji ambazo ni:
(b) chura hupitia hata zifuatazo za ukuaji:
(c) binadamu
hupitia hatua zifatazo za ukuaji
Hatua za ukuaji katika mwili wa binadamu
Ukuaji wa mwili wa binadamu umegawanyika katika hatua
mbalimbali. Hatua hizo ni utoto wa awali, utoto, ujana utu uzima na uzee. Kila
hatua huhusisha mabadiliko mahususi ya kimeumbile.
(a) Utoto wa awali
Hii ni hatua ya kwanza ya ukuaji wa binadamu ambayo huanzia pindi
mtoto anapozaliwa hadi kufikia miaka miwili. Hiki ni kipindi ambacho mtoto
amezaliwa na anaanza kujifunza vitu mbalimbali. Katika kipindi hiki mtoto
hujifunza kugusa, kutembea na kuwa na hisia. Kadri muda unavyoenda mtoto huanza
kushika kichwa, kukaa chini, kutambaa, kujizungusha na kutembea kwa hatua
chache bila msaada. Baada ya kufikia umri wa miaka miwili mtoto huanza kukimbia,
kupanda na kushuka katika vitu mbalimbali bila msaada. Pia, uwezo wa mtoto
kutunza kumbukumbu na kuzungumza huongezeka. Hisia za kukasirika, furaha,
huzuni na uoga ni baadhi ya tabia zinazoonekana katika hatua hii. Mtoto pia
hujifunza kupenda na kuamini watu hasa wanaomhudumia na kumjali. Meno ya
utotoni huanza kuota katika hatua hii.
(b) Utoto
Kipindi cha utoto huanzia kuanzia miaka miwili (2) hadi miaka
kumina tatu (13). Katika kipindi hiki mtoto huongezeka kimo na uzito, hii
huambatana na mabadiliko mengi katika miili yao. Katika hatua hii meno ya
utotoni hutoka na meno ya kudumu huota. Mtoto hujenga uwezo mkubwa wa kupanda
juu ya vitu mbalimbali, kuruka, kuendesha vitu mbalimbali, kukimbia, kula
mwenyewe, kuchora na kupaka rangi. Mtoto hujifunza kutekeleza mahitaji yake ya
kijamii kwa mfano kuvaa nguo, kula na kuoga mwenyewe. Katika kipindi hiki ukuzaji
wa maarifa hutegemea sana msaada wa wazazi au walezi. Pia, mahusiano kati ya
mtoto na wazazi au walezi ni muhimu sana katika kipindi hiki. Watoto wanatakiwa
kupata mlo kamili, mazingira mazuri ya kucheza, huduma bora za kiafya, usafi wa
mara kwa mara, mahali pazuri pa kulala na mavazi.
(c) Ukuaji wakati wa ujana
Hiki ni kipindi cha mpito kuelekea utu uzima. Kipindi hiki
kinahusisha kubalehe kwa kijana. Balehe ni kipindi kinachotambulika kama kipindi
cha mpito kutoka utoto kwenda utu uzima. Katika kipindi hiki, mabadiliko
makubwa ya kiakili, kimaumbile, kimahusiano na kitabia hutokea. Kipindi hiki
pia huchagizwa na vichocheo vya mwili yaani homoni zinazosababisha mabadiliko
ya kimwili na kiakili. Kwa kawaida wavulana huingia katika kipindi cha balehe
wanapofikia umri wa miaka 12 hadi 13 na wasichana huingia katika kipindi cha balehe
kati ya umri wa miaka 11 hadi 12. Baadhi ya wavulana na wasichana huwahi au
huchelewa kuliko muda wa wastani wa kuingia balehe. Hali hiyo ya kuwahi au
kuchelewa hutegemea sababu za kijenetiki, lishe na mazingira.
Mabadiliko ya kimaumbile wakati wa balehe
Msichana na mvulana huonesha mabadiliko mbalimbali wakati wa
balehe.
(a) Mabadiliko ya kimaumbile wakati wa balehe kwa msichana
Kwa upande wa msichana mabadiliko hayo humfanya msichana kuwa
na mwonekano.
Mabadiliko ya kimaumbile kwa msichana wakati wa
balehe hujumuisha:
(i) Kukua na kuongezeka kwa matiti.
(ii) Kuongezeka kwa utendaji kazi wa tezi za jasho.
(iii) Kuongezeka kwa ute katika uke.
(iv) Kukua kwa nywele za kwapani na sehemu zinazozunguka uke.
(v) Kuongezeka kwa kimo na uzito.
(vi) Sauti kubadilika na kuwa nyororo.
(vii) Kuota chunusi usoni.
(viii) Kupanuka kwa sehemu ya kiuno au nyonga.
(ix) Kupevuka kwa mayai na kuanza kupata hedhi au kuvunja
ungo.
Mzunguko wa hedhi
Hedhi ni mchakato wa asili wa kibaiolojia wa utokaji wa damu iliyochanganyika
na uteute kutoka kwenye ukuta wa uterasi kupitia uke. Hedhi ya mara ya kwanza
ni moja ya ishara ya msingi ya kubalehe kwa msichana. Hedhi hutokana na
kubomoka kwa utando na kuta za mji wa mimba, yaani uterasi. Kwa kawaida, hedhi
hutokea mara moja kwa mwezi
kama sehemu ya mzunguko wake ambapo yai moja au zaidi
hupevuka. Mzunguko wa hedhi ni kipindi kuanzia siku ya kwanza ya hedhi hadi
siku moja kabla ya hedhi inayofuata. Kwa kawaida mzunguko wa hedhi ni siku 28
kama Kielelezo namba 6 kinavyoonesha. Hata hivyo, kuna wanawake wengine wana
mzunguko wa kati ya siku 21 na 35.
Kielelezo: mzunguko wa hedhi wa siku 28
Kuanza kwa hedhi kunaashiria kubomoka kwa ukuta wa uterasi ambao
ulikuwa umejengeka kwa ajili ya kupokea zaigoti endapo yai lingerutubishwa.
Muda wa hedhi hutofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine. Kwa kawaida hedhi
hudumu kati ya siku 3 hadi 5. Ingawa, baadhi ya wanawake wanaweza kuwa na hedhi
fupi zaidi au ndefu hadi kufikia siku 7. Wakati wa hedhi vifaa maalumu
vinavyoitwa pedi za kike au taulo za kike hutumika kufyonza damu inayokuja
kupitia uke. Inashauriwa kutumia pedi za pamba. Pedi huvaliwa ndani ya chupi
kwa kutumia vibandiko au vibawa maalumu. Inashauriwa kubadilisha pedi mara kwa mara,
walau kila baada ya masaa matatu mpaka manne, ili kudumisha usafi na kuzuia
matatizo yanayoweza kutokea kama vile harara au maambukizi.
Kasoro katika mzunguko wa hedhi
Wakati mwingine kasoro hutokea katika mzunguko wa hedhi.
Miongoni mwa kasoro hizo ni hali ya kujisikia vibaya wakati wa mzunguko wa hedhi,
kukosa hedhi, maumivu makali wakati wa hedhi na kutokwa na damu nyingi kwa muda
mrefu. Kasoro hizi zinaweza kusababishwa na mabadiliko ya homoni, msongo wa
mawazo au matatizo ya kiafya.
Kujisikia vibaya wakati wa hedhi: Kwa baadhi ya wanawake hedhi huambatana
na kujisikia vibaya. Hii ni hali ambayo inaweza kumfanya mtu ashindwe kufanya
kazi zake kwa ufanisi katika kipindi cha hedhi. Athari za hali hii zinaweza
kuwa za saa chache na kwa wengine siku nyingi. Hali hii hutofautiana kati ya
mtu mmoja na mwingine. Hali hizo ni pamoja na sonona, hasira, mchafuko wa
tumbo, kuumwa kichwa, kizunguzungu, mapigo ya moyo kwenda kasi, kukosa hamu ya
kula na kujaa maji kwenye miguu, mikono na vidole. Ili kupunguza makali ya hali
hii inashauriwa kufanya mazoezi walau mara 3 hadi 5 kwa wiki. Pia, kula mlo
kamili ukijumuisha na matunda, kulala kwa muda wa kutosha na kupumzika.
Maumivu makali wakati wa hedhi: Baadhi ya wanawake hupata maumivu
makali wakati wa hedhi. Maumivu haya yanaweza kutokea tangu msichana anapo
balehe au huanza baadaye. Maumivu haya hutokea kutokana na kujifinya kwa kuta
za uterasi kutokana na uwiano usio sahihi wa homoni mwilini. Sababu nyingine
zinazoweza kusababisha maumivu wakati wa hedhi ni maambukizi ya magonjwa katika
mlango wa kizazi. Vilevile, husababishwa na uvimbe katika tumbo la uzazi na
maambukizi ya magonjwa katika mfumo wa uzazi. Matatizo haya yanaweza kumpata mwanamke
yeyote. Hata hivyo, wanawake wenye uwezekano mkubwa zaidi wa kupata tatizo hili
ni wale wanaovuta sigara, kunywa pombe, na wenye uzito mkubwa pamoja na wale
wanaofikia balehe wakiwa na umri mdogo wa kabla ya miaka 11.
Kutokwa damu nyingi kuliko kawaida: Baadhi ya wanawake hupata tatizo la
kutokwa na damu nyingi kuliko kawaida wakati wa hedhi. Wengine hupata hedhi
siku nyingi kupita siku za kawaida za hedhi. Kiwango hiki huweza kusababishwa
na damu kuto kuganda kwa muda mwafaka. Pia, kasoro katika mfumo wa homoni
zinaweza kusababisha mwanamke kutokwa damu nyingi kuliko kawaida wakati wa
hedhi.
(b) Mabadiliko ya kimaumbile wakati wa balehe kwa mvulana
Wakati wa balehe mvulana huwa na baadhi ya mabadiliko kama ifuatavyo:
(i) Kukua kwa korodani na uume.
(ii) Kuongezeka kwa utendaji kazi wa tezi za jasho.
(iii) Kukua kwa nywele za kwapani na kuzunguka sehemu za
siri, kifua, tumbo na ndevu kwa baadhi ya wavulana.
(iv) Kuongezeka kwa kimo na uzito.
(v) Sauti kubadilika kuwa nzito.
(vi) Kuota chunusi usoni kwa baadhi ya wavulana.
(vii) Kupata ndoto nyevu.
(viii) Kupanuka kwa misuli sehemu za kifuani na mikononi.
Mabadiliko ya kijamii wakati wa balehe
Katika kipindi cha balehe baadhi ya mabadiliko ya kijamii
yanayotokea kwa wasichana na wavulana ni kama yafuatayo:
(a) Kuanza kujitambua: Katika kipindi cha balehe
vijana wanaanza kujidadisi na kujitambua vizuri, kuwa ni wasichana au wavulana
na kuanza kujenga uhusiano wenye hisia.
(b) Kutaka kutambuliwa: Vijana katika kipindi hiki
huwa katika harakati ya kutaka kutambulika kwa nafasi zao katika jamii na dunia
kwa ujumla. Harakati hizi zinaweza kuathiriwa na jinsia, kundirika, tamaduni na
mategemeo ya familia.
(c) Kutaka kuwa huru: Katika kipindi hiki vijana huwa
wanataka kuwa huru na kujiamulia mambo yao wenyewe bila kuingiliwa na wazazi au
walezi. Hali hii mara nyingi husababisha migogoro kati ya vijana na wazazi au
walezi wao. Wazazi au walezi wana wajibu wa kuwaongoza vijana wao, lakini
vijana huona wana uhuru wa kuamua mambo yao. Vijana wana wajibu wa kutambua
nafasi ya wazazi au walezi na kuwa na uhuru wenye mipaka.
(d) Kutaka kujifunza mambo mapya: Vijana wakifikia
kipindi cha balehe, hupenda kujifunza mambo mbalimbali mapya na kujaribu vitu
mbalimbali. Hali hii huwasababisha kuingia katika tabia hatarishi katika
maisha. Katika kipindi hiki vijana hupenda kujifunza stadi mbalimbali kama
kuendesha gari na pikipiki. Pia, baadhi ya vijana huanza kuvuta sigara au
kutumia dawa za kulevya. Tabia hii husababisha kuanza kufanya ngono, hivyo
kusababisha mimba zisizokusudiwa au maambukiz: ya virusi vya UKIMWI na magonjwa
ya ngono.
Mabadiliko ya kiakili wakati wa balehe
Katika kipindi cha balehe wasichana na wavulana huwa na
mabadiliko ya kiakili. Mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo:
(a) kutambaa mambo yanayowazunguka katika uhalisia wake.
(b) kujenga stadi za kutafuta matatizo magumu na yenye utata.
(c) kuelewa mawazo ya mtu mwengine.
(d) Kupuuza athari za beachi ya matendo wanayofanyafanya.
Mabadiliko ya kimahususi wakati wa balehe
Wakati wa balehe wasichana na wavulana huonesha mabadiliko
katika uhusiano wao na jamii inayowazunguka. Mabadiliko hayo ni kama yafuatayo:
(a) Kupenda kukaa na marafiki kwa muda mrefu kuliko familia:
Katika kipindi hiki kijana huona marafiki zake ni wa muhimu
zaidi kuliko wazazi, walezi au ndugu zake. Hushiki kwamba marafiki zake
wanamweleza zaidi kwa kuwa mawazo yao yanadendana. Hivyo, huona ni vyema kukaa
na vijana wenzake kuliko wazazi, walezi au ndugu zake.
(b) Kuwa na mitazamo tofauti na watu wazima:
Haii li inatokana na kupenda kujenga mitazamo yake mwenyewe
na kuhoji kila anachokiona na kukisikia. Huthofu kuigana mambo yake arayo nae
na hali. Kwa kawada mitazamo hii húsababisha migogoro kati ya kijana na wazazi,
walezi au ndugu zake. Hali hiyo, migogoro hii haina halirafiki uhusiano kati ya
kijana, mzazi, mlezi au ndugu kwani ni hali ya mipito tu.
(c) Kupenda
kushindana: Hiki ni
kipindi ambacho vijana hupenda kushindana na kuigizanisha na wenziwa katika
masuala mbalimbali. Wanapenda kuonekana kwao wao wanafanya vizuri katika kila
jambo nyumbani na hata nje ya nyumbani. Hupenda kuonekana kama mfano wa kuiga.
Mabadiliko ya kihisia
Mabadiliko yanayotokea katika hisia za wasichana na wavulana
katika kipindi hiki cha balehe ni kama yafuatayo:
(a) Kuonesha hisia kali na za ndani
katika nyakati tofauti: Hisia
za vijana katika kipindi hiki hubadilishana mara kwa mara. Jambo dogo linaweza
kumharibisha, kumkushirisha au kumisimisha. Katika kipindi hiki mshoneno au
mvutano anaeza kulia au kuwa na hasira kali kutokana na jambo dogo dogo. Hali
hii ya kawada kwa vijana au hubadilishana na hali ya ubongo au wakijana kuwa
machakato au kutaka kuonesha hisia katika hali ya utu uzima. Jambo hili
linaweza kuongeza migogoro ya mara kwa mara katika familia na jami anaoishi
endapo hawalimwelewa na kujaa naye taratibu.
(b) Kuonesha kujipendelea zaidi: Katika kipindi hiki kijana anaijali
zaidi kuliko watu wengine. Anapenda kuonekana vyema vizuri kimaumbile na
kimawazo. Pia, anaeza kujilingisha umbo lao na maumbo ya vijana wa kundirika
moja au kundirika lingine. Hii ndiyo ‘shabubu’ vijana wengi huiga watu
wanaowaza ni maafufu namna ya kuvaa, kunywa, kuonekana na hata kutembea.
Nja za kuhimili mabadiliko yanayotokea walafu
wa balehe
Mabadiliko yanayotokea wakati wa balehe kwa mischana na
mfululano hayepeki. Hata hivyo, kuna mbinu mbali mbali zinazoweza zikifuatwa
ipasavyo zingazweza kupunguza au kuondoa changamoto zinazozambatana na
mabadiliko hayo. Ili kupunguza athari zinazotokeza kutoka wakati wa balehe
inashauriwa kufanya mambo yafuatayo:
Kufanya mazoezi:Wakati wa balehe kijana hukua haraka na kuongezeka
uzito na hivyo kwa wa nguvu nyingi. Mazoezi yanasaidia mzunguko wa damu na hewa
ya oksijeni na hivyo hufanya mwili kuchangamka na kuondoa msongo au mawazo na
kujiskia furaha.
Kula chakula mizuri na kutosha na kula na kamili: Kulala usingizi kwa muda wa kutosha
unahumu mwili kuwa mwil uunacuk. Usingizi wa kutosha husaidia kuondoa uchovu na
kusawazisha viwango vya nishati. Lishe bora inayochukua vyakula vyenye
virutubisho muhimu huchangia katika ukuaji wa afya ya mwili na akili.
Kuepuka matumizi ya pombe, tumbaku na vilevi vingine: Vilevi huathiri utendaji wa mfumo
wa fahamu na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi. Kwa kuwa katika kipindi hiki kuna
changamoto za kushindwa kufanya maamuzi mawili. Inashauriwa kuepuka kutumia
vilevi na badala yake kufulia mtindo wa maisha afya bora. Pia, ni vyema
kudumisha heshima kwa wengine ili kukuzia maadili mema.
Kushirikiana marafiki au ndugu katika changamoto
wanazopitia:
Changamoto marafiki au balehe humkusha kila kijana kwa hamna yake. Mara
nyingine kijana hudhani kwa na yeye tu anaepukana na hali hiyo. Mawazo hayo
huongeza mehemko, wasiwasi na kutojaliwa. Kushirikisha kijana katika changamoto
wanazopitia, husaidia kupata ushauri sahihi kuhusu namna ya kukabiliana na
changamoto wanazopitia.
Kuomba msaada kwa watu au kuamini: Wakati mwingine katika kipindi cha
balehe, vijana hupta changamoto pa kushindwa kukabiliana nazo. Ni muhimu kuomba
msaada kutoka kwa walezi, walimu, watu wengine wanaoona.
Kuzingatia usafi wa mwili: Usafi wa mwili ni muhimu katika
kipindi cha balehe. Usafi huo ni kama kuoga, kufua nguo, kupiga pasi na kunywa
nywele. Kwa wasichana ni muhimu kubadilisha kwa wakati taulo za kute
wanazozivaa wakiwa na hedhi.
(d) Utu uzima
Hatua ya utu uzima ni kipindi ambacho ukuaji wa mwili hufikia
kimo mo au huendelea kukua taratibu. Mwili wa binadamu hutumia nguvu zedi
kudumisha afya ya mifumo yake kuiko kuongezeka kwa uzima. Kipindi hiki
kinatokaeza umriza mika 18-65. Katika kipindi hiki cha utu uzima ukuaji unakuwa
huweza mishwio na uwezo wa kazi, hua huwa umekamilika. Mtu umriza huweza
kuijamini na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi na kuwaijika katika masuala
mbalimbali za kimaisha, ufanayi wa mazoezi, mi kamili, mavazi na malazi safi.
(e) Uzee
Kipindi hiki cha uzee huanzia miaka 65 na kuendelea. Katika
kipindi hiki mifumo ya mwili huzorota na mwili kudhoofika ukilinganisha na
ujana. Uwezo wa nguvu za mwili hupungua, mvi hutokea na uwezo wa kushika
hubunguka. Ngozi hujanibisha na uwezo wa kutunza kumbukumbu hupungua. Wazee
hujaliwa mafunzo wa kuhusu usafi, ulaji wa mlo kamili, na ufanyaji wa mazoezi
mepesi. Uangalizi wa afya kwa mara kwa mara ni muhimu ili kuweka afya zao
vizuri.
SURA YA TATU: MFUMO WA UZAZI
Dhana ya mfumo wa uzazi wa binadamu.
Kuzaliana ni mchakato wa kibaolojia ambapo viumbehai
hutengeneza uzao mpya. Kuzaliana huongeza idadi ya viumbe na kuhakikisha uwepo
wa spishi. Kuzaliana huendelea kuwepo kuliko kizazi kinjia hadi kingine. Kuna
aina mbili za kuzaliana, ambazo ni uzao wa nje na ujamiwa hadi uzao. Uzao wa
nje ni wa kutokujamiiana (nafasi). Kuzaliana kwa nje ni ya kujamiiana
kunahusisha wazazi wawili (wa kiume na kike) na kuungana kwa seli za uzazi zao
ili kuumba ya yai la mwanamke ili kutengeneza uzao mpya. Kwa upande mwingine,
kuzaliana bila ya kujamiiana kunahusisha mzazi mmoja tu na hutengeneza uzao
mpya wananaofana kabisa na mzazi huyo. Binaadamu na viumbe veringine, kuzaliana
huevezesha na mfumo wa uzao.
Mfumo wa uzazi ni mkusanyiko wa ogani za michakato
inayohusika na uzalishaji wa viumbehai. Kwa binadamu, mfumo wa uzazi unaweza
kugawanyika katika sehemu mbili wa kumbembe na wa kike ambapo kila mmoja una
ogani maalumu zinazofanya ili kuwezesha uzazi. Uzazi kwa binadamu huwezekana
baada ya kubaliana. Kifendo cha uzalishi kwa binadamu kinahusisha utengenezaji
wa gameti. Gameti zime utengenezwa ndani ya korodani na gameti uke au yai
hutengenezwa ndani ya ovari.
Mfumo wa uzazi unafadhiliwa na vichocho au homoni kama vile
oestrogeni, projestroni, na testosteroni, ambazo zina jumla la kudhibiti ukubwa
wa uzazi kwa uzazi, mzunguko wa hedi, uzalishaji wa gameti ya mwanamke. Mfumo
huu ni muhimu kwa binadamu kwani husababisha ongezeko la idadi ya vyumbehai
jamii. Hivyo, husaidia kuwepo kwa mwendoleo wa vizazi. Pia, huwezesha
kurithisha sifa zao na kuchangia katika kuendelea kwa vinasaba kutoka kizazi
kimoja hadi kingine.
Mfumo wa uzazi wa binadamu
Mfumo wa uzazi wa mwanaume.
Mfumo wa uzazi wa mwanaume una sehemu kuu mbili ambazo ni
sehemu za nje na sehemu za ndani. Sehemu za nje zimeundwa na uume na korodani.
Sehemu za ndani zimeundwa na mirija ya manii, urethra, kifuko cha manili, tezi
dume na tezi za kopa. Kielelezo namba 1 kinaonesha shemu za ndani na za nje za
mfumo wa uzazi wa mwanaume.
Kielelezo: mfumo wa uzazi wa mwanaume
Jedwali: sehemu za mfumo wa mwanaume na kazi zake
|
No |
sehemu |
maelezo |
Kazi |
|
1 |
korodani |
Hupatikana ndani ya mfuko wa ngozi. Korodani huning'inia nyuma ya uume. Kila mwanaume ana jozi ya korodani. |
- Kutengeneza gameti ume na kuzihifadhi - Kuzalisha homoni ya testosteroni, inayohusika na mabadiliko ya maumbile kama vile ukuaji wa ndevu, sauti kuwa nzito, na misuli yenye nguvu katika kipindi cha balehe. |
|
2 |
Mirija ya manii |
Mrija uliojizungusha unaonganisha korodani na urethra. |
Kuhifadhi na kusafirisha mbegu za kiume (gameti ume) kutoka kwenye korodani hadi kwenye urethira. |
|
3 |
uume |
Ni mrija mwembamba unaopatikana ndani ya uume na hupita kutoka kwenye kibofu cha mkojo hadi kwenye ncha ya uume. |
- Kusafirisha mbegu za kiume
zilizochanganyika na majimaji ya manii kwenda kwenye mfumo wa uzazi wa
mwanamke. - Kusafirisha mkojo kutoka kwenye
kibofu cha mkojo hadi nje ya mwili. |
|
4 |
urethira |
Ni mrija mwembamba unaopatikana ndani ya uume na hupita kutoka kwenye kibofu cha mkojo hadi kwenye ncha ya uume. |
- Kusafirisha mbegu za kiume zilizochanganyika na majimaji ya manii kwenda kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke. - Kusafirisha mkojo kutoka kwenye kibofu cha mkojo hadi nje ya mwili. |
|
5 |
Kifuko cha manii |
Ni jozi ya ogani ndogo za mfumo wa uzazi wa mwanaume zilizopo karibu na tezi dume, nyuma ya kibofu cha mkojo. |
Kutengeneza na kutoa majimaji yenye virutubisho ambavyo hutoa nishati kwa mbegu za kiume ili ziweze kuogelea kuelekea yai la mwanamke. |
|
6 |
Tezi dume |
Ni ogani inayopatikana chini ya kibofu cha mkojo, ikizunguka sehemu ya juu ya urethira. |
Kutoa majimaji mazito yenye utelezi ambayo husaidia kulinda na kujongea kwa kuogelea tezi kopakwa mbegu za kiume. |
|
7 |
Tezi kopa |
Ni jozi ya ogani zinazopatikana chini ya tezi dume |
Kutoa majimaji yanayosaidia kupunguza asidi katika urethira, ili kuandaa upitishaji wa mbegu za kiume. |
Mfumo wa uzazi wa mwanamke
Mfumo wa uzazi wa mwanamke ni mfumo unaohusika na uzalishaji
wa mayai au gameti uke, utoaji wa homoni, na kutoa mazingira ya kutungwa kwa
mimba na ukuaji wa mtoto. Mfumo huu umeundwa na sehemu kuu nne, ambazo ni
ovari, mirija ya falopio, uterasi na uke. Mfumo wa uzazi wa mwanamke unadhibitiwa na
homoni za estrogeni and projesteroni, zinazosaidia mzunguko wa hedhi, mimba na
mchakato wa kuzaa.
Kielelezo: mfumo wa uzazi wa mwanamke
|
Na |
Sehemu |
Maelezo |
Kazi |
|
1 |
Ovari |
Ni jozi ya tezi za uzazi zilizopo upande wa kulia na kushoto Wwa uterasi. |
- Kutengeneza na kuhifadhi gameti uke au ova.
- Kutoa homoni muhimu kama oestrojeni na projesteroni, ambazo husaidia kudhibiti mzunguko wa hedhi, ukuaji wa ogani za uzazi na kuwezesha ujauzito. Homoni hizo pia zinahusika na mabadiliko mbalimbali kwa msichana wakati wa balehe. |
|
2 |
Mirija ya falopio |
Ni mirija miwili inayopatikana upande wa kushoto na kulia mwa mji wa mimba (uterasi). Mirija hii huunganisha ovari na uterasi. |
- Kusafirisha yai kutoka kwenye ovari hadi mji wa mimba. Pia, husaidia katika kuvuta na kuelekeza yai kuelekea mji wa mimba.
- Ni sehemu ambayo urutubishaji wa yai hufanyika. |
|
3 |
Uterasi (mji wa mimba) |
Ni mfuko wenye kuta za misuli minene. Wakati wa mimba, kijusi hukua na kukomaa ndani ya uterasi hadi wakati wa kujifungua. |
- Kutoa mazingira ya kukua kwa kijusi wakati wa ujauzito. - Kutengeneza mji wa mimba |
|
4 |
Mlango wa kizazi |
Ni sehemu ya chini ya mji wa mimba (uterasi) inayounganisha uterasi na uke. |
- Kudhibiti na kuruhusu mtiririko wa damu wakati wa hedhi.
- kupokea mbegu za kiume na kutoa njia ya kupita mtoto wakati wa kujifungua. |
|
5 |
Uke |
Ni sehemu inayopatikana kati ya shingo ya kizazi nasehemu za nje za mwili. |
- Kupokea mbegu za kiume. - Kupitisha mtoto wakati wa kujifungua. - Kutoa njia ya damu wakati wa hedhi. - Hulinda viungo vya uzazi dhidi ya maambukizi, kwani hutoa mazingira ya asidi ambayo yanazuia bakteria hatari. |
Kasoro katika mfumo wa uzazi
Kasoro katika mfumo wa uzazi ni hali au changamoto zinazoweza
kuathiri uwezo wa mfumo wa uzazi wa kike au wa kiume kufanya kazi ipasavyo.
Kasoro hizi zinaweza kuwa za kimaumbile au za kiafya. Kasoro hizi zinaweza kuwa
za kurithi, mitindo mibaya ya maisha, lishe duni, magonjwa sugu au athari za
kimazingira kama vile kemikali na mionzi hatari. Aidha, uchunguzi wa mara kwa
mara na matibabu ya mapema ni muhimu ili kuzuia au kurekebisha matatizo na
kasoro katika mfumo wa
uzazi wa mwanaume na mwanawake.
Kasoro katika mfumo wa uzazi wa mwanaume
Kasoro katika mfumo wa uzazi wa mwanaume ni changamoto
zinazoweza kuathiri utendaji wa kawaida wa mfumo wa uzazi. Baadhi ya kasoro
hizo ni kama ifuatavyo:
Ugumba
Hii ni hali ya mwanaume kushindwa kurutubisha yai la kike, na
hivyo kushindwa kutungisha mimba. Ugumba kwa mwanaume husababishwa na mambo
mbalimbali ikiwemo kutoa mbegu chache, hivyo kupunguza uwezekano wa kulifikia
na kurutubisha yai. Pia, kuwa na mbegu dhaifu zisizo na uwezo wa kuogelea
kuiifikia yai. Kuzalisha mbegu zenye upungufu kwa mfano mbegu zilizokosa mkia,
kuwa na mikia miwili, kukosa kichwa au kuwa na umbo lisilo la kawaida.
Vilevile, korodani zinaweza kushindwa kutengeneza mbegu za
kiume kutokana na magonjwa, lishe duni au upungufu wa homoni. Sababu nyingine
ya ugumba ni mirja ya mani kuziba kutokana na magonjWaya ngono kama vile
kisonono na kaswende.
Matatizo ya tezi dume
Hii i hali inayohusiana na uharibifu au kupanuka kwa tezi dume.
Kasoro hizi zinaweza kuwa na madhara kwenye mfimo wa mkojo na uzazi. Kupanuka
kwa tezi dume hutokana na maambukizi ya magonjwa au saratani. Tatizo hii
hupelekea kuziba kwayUrethira fia kusababisha kukojoa kwa shida.
Kasoro katika mfumo wa uzazi wa mwanamke
Kasoro katika mfumo wa uzazi wa muanamke fii changamoto
zinazoweza kuathiri utendaji wa kawaida wa mfumo wa uzazi. Baadhi ya kasoro
hizo ni kama ifuatavyo:
Ugumba
Ni hali ya mwanamke Kushindwa kupata mimba kwa sababu
mbalimbali. Ugumba husababishwa na'mambo mbalimbali ikiwemo mayai kushindwa kupevuka.
Hali hii hutokana na matatizo ya utoaji wa homoni za oestrojeni au
projesterofi.
Aidha, ugumba,unaweza kusababishwa na maambukizi ya magonjwa ya
ngono kama kisonono, kaswende na pangusa. Magonjwa haya husababisha kuziba kwa
mirja ya kupitisha mayai ili yarutubishwe. Magonjwa haya yanaweza kuifanya
mirija iwe myembamba au iwe na makovu hivyo kuzuia yai lisiweze kupita.
Kasoro katika shingo ya mlango wa kizazi
Shingo ya miango wa kizazi inaweza kupata madhara kutokana na
matatizo ya uzazi au maambukizi katika shingo ya miango wa kizazi. Hali hii
inaweza kusababisha shingo ya kizazi kuwa na kasoro.
Kasoro za hedhi
Hizi ni kasoro zinazotokana na muda, kiwango cha damu
inayotoka au kujisikia vibaya wakati wa hedhi. Moja ya kasoro ni kukoma au
kutopata hedhi kwa mwanamke asiye na ujauzito kwa muda fulani. Kasoro nyingine ni
pamoja na kupata maumivu makali wakati wa hedhi kutokana na kukaza kwa misuli
ya uterasi. Pia, baadhi ya wanawake hupata shida ya kutokwa na damu kwa muda
mrefu kuliko kawaida wakati wa hedhi. Kasoro hizi husababishwa na matatizo ya
uzalishwaji wa homoni, hasa upungufu wa utolewaji wa homoni ya oestrojeni,
matatizo ya kijenetiki, magonjwa sugu, na sonona. Kasoro hizi zinaweza kutibiwa
na hivyo ni muhimu kupata ushauri wa kitabibu.
Utunzaji wa mfumo wa uzazi
Mfumo wa uzazi ni muhimu kwa ustawi wa binadamu. Hivyo ni
muhimu kutunza mifumo ya uzazi ili kuepukana na madhara yanayoweza kutokea na
kuharibu au kupunguza ufanisi wake. Madhara hayo ni kama vile maambukizi katika
sehemu za uzazi yanayopelekea magonjwa. Mfano wa magonjwa ya mifumo ya uzazi ni
kama vile magonjwa ya zinaa, maambukizi ya fangasi, bakteria na vijidudu
vingine kwenye via vya uzazi. Ili kutunza mifumo ya uzazi tunapaswa kufanya
yafuatayo:
Kuzingatia usafi
Ni muhimu kuzingatia usafi wa mwili kwa kuoga kwa maji safi
na sabuni kila siku. Pia, ni muhimu kusafisha sehemu za siri kila mara
unapotoka kujisaidia kwa kutumia maji safi. Vilevile, kutumia vyoo visafi na
kuzingatia usafi chooni ni muhimu katika kulinda mifumo ya uzazi. Kuvaa nguo za
ndani zilizo kavu na safi kila siku pamoja na kuepuka kuchangia nguo za ndani
na mtu mwingine ili kuepuka maambukizi.
Kuzingatia lishe bora na mazoezi
Kupata lishe bora yenye virutubisho vinavyotakiwa katika
uwiano sahihi na kunywa maji ya kutosha kunasaidia kutunza mifumo ya uzazi.
Pia, kufanya mazoezi mara kwa mara kunasaidia kuimarisha mwili na mifumo yake.
Mazoezi yanasadia pia kuepuka uzito uliopitiliza ambao huweza kuathiri mwili na
mfumo wa uzazi.
Kuepuka tabia hatarishi
Baadhi ya tabia ni hatarishi kwa afya ya mwili wa binadamu.
Utumiaji wa pombe, sigara na vilevi vingine huzorotesha afya ya mwili na mifumo
ya uzazi pia. Ni vema kuepuka tabia hizi ili kuwa na mfumo wa uzazi ulio na afya.
SURA YA NNE: USUMAKU
Dhana ya usumaku
Usumaku ni uwezo wa sumaku kuvuta au kusukuma vitu. Sumaku
hutumia uwezo huu kuvuta vitu vyenye asili ya chuma. Kwa hivyo, sumaku ni kifaa
ambacho kina uwezo wa kuvuta vitu vyenye asili ya chuma. Kila sumaku ina ncha
mbili. Ncha hizo ni ncha ya Kaskazini (KAS) na Kusini (KUS). Sumaku huzalisha
uga wa sumaku. Uga wa sumaku ni eneo linazunguka sumaku ambalo kani ya sumaku
huhisiwa. Kani ya sumaku ndiyo inayosababisha vitu kuvutwa au kusukumwa na
sumaku. Kwa hiyo, kani ya sumaku kuvuta au kusukuma husababishwa na usumaku.
Pia, kani ya sumaku huwakilishwa na mistari ya kufikirika inayoitwa mistari ya
kani ya sumaku ambayo huonekana unaposambaza unga wa chuma kuzunguka sumaku
mche mstatili. Unga wa chuma hujipanga kwa muundo maalum na kuunda mistari.
Maumbo ya sumaku
Sumaku inaweza kuonekana katika maumbo mbalimbali kulingana
na matumizi yake. Mifano ya maumbo ya sumaku ni kama vile sumaku mche mstatili,
sumaku kwatofarasi, sumaku U, sumaku duara na sumaku mche duara. Kila umbo
huathiri jinsi sumaku inavyounda eneo la usumaku. Pia, umbo la sumaku huathiri
matumizi
Yake.
Kielelezo: maumbo ya sumaku
Sifa za sumaku
Sumaku zina sifa mbalimbali muhimu
ambazo huelezea tabia zake. Baadhi ya sifa hizo ni:
(a) Sumaku huvuta vitu vyenye asili
ya chuma.
(b) Kani ya sumaku ni kubwa kwenye
ncha za sumaku.
(c) Sumaku mbili zikikaribiana, ncha
zinazofanana hukwepana na ncha zisizofanana huvutana.
Umbo la sumaku huathiri uwezo wa
sumaku kuvuta vitu. Pia, ncha za sumaku zina kani kubwa zaidi ya kuvuta vitu
kuliko sehemu zingine za sumaku, ambazo huwa zina kani ndogo ya kuvuta vitu.
Kanuni ya usumaku
Kanuni ya msingi ya usumaku inasema
"Ncha za sumaku zinazofanana hukwepana na ncha zisizofanana huvutana".
Unaposukuma ncha mbili za kaskazini
za sumaku kwa kuelekea, kani ya sumaku husukuma ncha hizo zisigusane. Hii ni
kwa sababu nguvu za sumaku zinakwepana. Kwa upande mwingine, ncha ya kaskazini ya
sumaku moja huvuta ncha ya kusini ya sumaku nyingine. Kazi hii inadhihirisha
Kanuni ya usumaku.
Matumizi ya sumaku
Sumaku hutumika sehemu mbalimbali kama vile nyumbani, shuleni, hospitalini na viwandani. Yafuatayo ni baadhi ya matumizi ya sumaku. Kunyanyua vitu vizito Sumaku hutumika kuinua vitu vilivyo na asili ya chuma. Vitu hivyo vinaweza kuhamishwa kutoka sehemu moja hadi sehemu nyingine. Bandarini, sumaku pia hutumika katika upakiaji na upakuaji wa mizigo yenye asili ya chuma.
Kielelezo: sumaku ikiwa imenasa na kunyanyua
mzigo
Matengenezo ya vifaa
vya kielektroniki
Fundi simu, redio na kompyuta hutumia
bisibisi na zana nyingine zenye sumaku kunasa skrubu ndogo za kufungia simu,
redio au kompyuta. Kielelezo namba 9 kinaonyesha skrubu iliyonaswa na bisibisi
yenye sumaku.
Kielelezo: bisisbisi yenye sumaku ikiwa imenasa
skrubu
Kutengeneza kengele ya
umeme
Sumaku hutumika kutengeneza kengele
za umeme. Unapobonyeza kengele mkondo wa umeme huzalisha kani ya usumaku.
Hivyo, kani ya usumaku husababisha kugongwa kwa kengele na kutoa mlio.
Kuonesha uelekeo
Dira ni kifaa chenye sumaku ambacho
huonesha mwelekeo wa upande wa kaskazini na kusini wa dunia. Dira hutumika
kuongoza watu kutambua pande kuu za dunia. Vilevile, hutumika kumwongoza
nahodha wa meli na rubani wa ndege kwenda mwelekeo sahihi.
Kielelezo: Dira
Kuzalisha umeme
Sumaku hutumika kuzalisha umeme.
Dainamo ya baiskeli ina sumaku ambayo imezungukwa na koili. Gurudumu la baiskeli linapozunguka husababisha
sumaku pia kuzunguka. Mzunguko wa sumaku huzalisha umeme kwenye koili. Umeme
huo husafirishwa kwa waya kwenda kwenye taa na kusababisha taa hiyo kuwaka.
Magurudumuya baiskeli yanapozunguka kwa kasi, umeme unaozalishwa huongezeka na
taa huangaza zaidi. Magurudumu ya baiskeli yanapozunguka polepole,umeme
hupungua na mwanga wa taa huwa hafifu.
Kielelezo: sumaku kwenye dainamo ya baiskeli
Kutenganisha vitu
Sumaku hutumika kutenganisha vitu
vyenye asili ya chuma na visivyo na asili ya chuma. Mbinu hii hutumika katika
viwanda vya vyakula, kutenganisha chembechembe za chuma kutoka kwenye bidhaa za
chakula. Hii husaidia kuhakikisha usalama na kuzuia uchafuzi wa chakula.
Kielelezo: sumaku ikitengamnisha chembechembe
za chuma kutoka kwenye unga
Sumaku hutumika pia katika vifaa mbalimbali vya kielektroniki na kiteknolojia. Baadhi ya vitu hivyo ni friji, redio, simu, kompyuta, jenereta, kadi za benki, vinasa sauti na vipaza sauti.
Utunzaji wa sumaku
Sumaku hupoteza kani pale ambapo ncha
zake zitavutana na kuvurugampangilio wa chembechembe zilizo ndani ya sumaku.
Sumaku hutunza kani yake kwa muda mrefu ikiwa tutazingatia yafuatayo:
(a) Kuweka sumaku mahali ambapo
hazitachangamana na vitu vyenye asili ya chuma.
(b) Hakikisha kuwa ncha za sumaku
zinazofanana hazielekeani.
(c) Kutoichoma moto sumaku.
(d) Kutoweka sumaku karibu na vitu
vyenye usumaku mkubwa zaidi au umeme.
(e) Kutoponda au kugongagonga sumaku.
SURA YA TANO: USIMBIKAJI KATIKA KOMPYUTA
Muundo wa kudhibiti
mlolongo
Katika muundo wa kudhibiti mlolongo,
maelekezo ya programu hufanyika
kwa mpangilio maalumu, hatua moja
baada ya nyingine. Hii inamaanisha
kuwa, maelekezo ya hatua ya kwanza
hufanyika kwanza, kisha ya pili,
hadi ya mwisho.
Mfano mzuri wa kazi ambayo hufanyika
kwa hatua ni uzalishaji wa mazao
shambani. Katika kupanda mazao
shambani hatua zake ni:
1. Kuandaa shamba;
2. Kupanda mbegu;
3. Kupalilia; na
4. Kuvuna.
Zingatia kuwa, hatua hizi ni lazima
zifuatwe kwa mpangilio huo ili kukamilisha kazi. Kwa mfano, huwezi kupanda
mbegu kabla ya kuandaa shamba, kwa sababu mbegu hazitaota.
Hii dhana ya kufanya kazi kwa kufuata
mlolongo hutumika pia kwenye programu za kompyuta. Kwa mfano, katika programu
ya Scratch, tunatumia muundo wa kudhibiti mlolongo kwa kupanga bloku za
maelekezo kutoka juu kwenda chini. Kompyuta itafuata maelekezo hayo katika
mlolongo huo.
Vibadilika na opereta
Programu nyingi za kompyuta
tunazotumia kila siku hufanya hesabu mbalimbali. Mfano, programu za kompyuta
zinatumika benki na maduka makubwa kufanya hesabu zinazohusisha fedha na
bidhaa. Fikiria umetembelea duka kubwa, ukanunua kalamu 3 kwa shilingi 300/=
kila moja, rula moja kwa shilingi 500/= na pipi 2 kwa shilingi 100/= kila moja.
Ukilipa kwa noti ya shilingi 2000/=, programu ya duka itahesabu jumla ya fedha
unayotakiwa kulipa (yaani shilingi 1600/=) na pesa za kukurudishia kama chenji
(yaani shilingi 400/=). Muhtasari wa taarifa za mfano huu
zimeoneshwa kwenye Jedwali lifuatalo.
Jedwali: Orodha ya manunuzi
|
Aina ya bidhaa |
idadi |
Bei ya kila bdhaa (shilingi) |
Jumla ndogo (shilingi) |
|
Kalamu |
3 |
300/= |
900/= |
|
Rula |
1 |
500/= |
500/= |
|
Pipi |
2 |
100/= |
200/= |
|
Jumla |
|
|
1600/= |
Katika mfano huu, kila bidhaa ina
idadi na bei. Ili programu ya kompyuta iweze kufanya hesabu hizi, inahitaji
njia ya kuwakilisha vipimo hivyo (idadi
na bei). Njia hiyo ni kutumia
vibadilika. Programu ya kompyuta inaweza kuwa na idadi yoyote ya vibadilika. Kila
kibadilika kinatambulika kwa jina na kinaweza kuwa na kiasi tofautitofauti
pindi programu inapoanzishwa na kuendelea kufanya kazi. Mifano ya vibadilika
tunavyoweza kuviunda kutoka katika mfano huu ni IdadiYaKalamu (thamani = 3),
BeiYaKalamu (thamani = 300) na BeiYaRula (thamani = 500). Inashauriwa
unapopendekeza jina la kibadilika, pendekezajina litakalo kukumbusha kipimo
kinachowakilishwa. Programu ya Scratch inaruhusu kuunda na kutumia vibadilika.
Kabla ya kutumia kibadilika, unatakiwa ukiunde. Umalizapo matumizi ya
kibadilika, unaweza kukifuta.
Kibadilika kikishaunndwa kinaweza
kutumika sehemu mbalimbali kwenyeprogramu. Rejea mfano wa kutumia programu za
kompyuta kwenye maduka makubwa, vibadilika vinaweza kutumika kutafuta jumla
ndogo ya kila bidhaa, jumla kuu ya bidhaa zote pamoja na chenji utakayopokea. Mfano,
kutafuta jumla ndogo ya kalamu, hesabu inaweza kuwakilishwa kama BeiYaKalamu *
IdadiYaKalamu. BeiYakalamu na IdadiYakalamu vinawakilisha bei ya kila kalamu
(ambayo ni shilingi 300) na idadi ya kalamu (ambayo ni 3) mtawalia.
Zingatia kwamba katika mahesabu,
operata ya * imetumika kuwakilisha kuzidisha badala ya alama x inayotumika
katika hisabati. Opereta nyingine unazoweza kutumia ni: kujumlisha (+), kutoa
(-), kugawanya (/), na mabaki (%).
Mbali na opereta za sayansi ya namba,
programu pia hutumia opereta za kulinganisha kama vile: ndogo kuliko (<),
kubwa kuliko (>) na sawa na (=). Pia kuna opereta za kimantiki ikiwa ni
pamoja na: na, au na si.
Kazi za kufanya zifuatazo zinaonesha namna ya
kutumia vibadilika na opereta katika kufanya hesabu.
Muundo wa kudhibiti
marudio
Baadhi ya kazi zinahitaji kitendo
fulani kurudiwa mara kadhaa kabla ya kupata matokeo ya mwisho. Katika usimbaji
hili linajulikana kama marudio au vitanzi. Rejea kazi zifuatazo kwenye mchezo:
(a) Kusogeza kihusika hatua kumi
kwenda kulia.
(b) Kusogeza kihusika kwenda kulia
mpaka kiguse ukingo.
(c) Kuchezesha sauti wakati mchezo
ukiendelea.
Kazi zote hizi zinahitaji kitendo
kurudiwa mara kadhaa kabla ya kupata matokeo ya mwisho. Kazi ya kwanza
inahitaji kusogeza kihusika hatua kumi kwenda kulia, utarudia kusogeza kihusika
hatua moja baada ya nyingine hadi zifike kumi. Kwa kazi ya pili, unahitaji
kusogeza kihusika kwenda kulia mpaka kiguse ukingo. Kwa kazi ya tatu, unahitaji
kuchezesha sauti wakati mchezo ukiendelea, sauti inapaswa kurudiwa bila
kumalizika mpaka mwisho. Kazi ya kwanza na ya pili kitendo kinachojirudia ni
nenda hatua moja kulia na ya tatu kitendo kinachojirudia ni kucheza sauti.
Utabaini kuwa, kwenye mfano wa
kwanza, kitendo kinarudiwa kwa idadi maalum (mara kumi). Katika mfano wa pili,
kitendo kinarudiwa mpaka jambo fulani litokee (kihusika kiguse ukingo). Kwenye
mfano wa tatu, kitendo kinarudiwa bila kikomo hadi mchezo uishe.
Hii inamaanisha kuwa kuna aina tatu
za kurudiwa kwa kazi kwenye programu, ambazo ni rudia ( ), rudia hadi ( ) na
milele. Kwa kitanzi cha rudia ( ), thamani iliyo ndani ya mabano inaonyesha ni
mara ngapi kitendo kitajirudia. Kwa kitanzi cha rudia hadi ( ), thamani ndani
ya mabano inaonyesha sharti litakalosababisha kitanzi kisimame. Kitanzi cha
milele kitaendelea kutekelezwa bila kikomo hadi utakaposimamisha mwenyewe au
kutumia kizuizi cha komesha. Katika Scratch, vitanzi hivi vinapatikana kwenye
bloku za Kidhibiti.
Kielelezo: aina za vitanzi katika scratch
Muundo wa kudhibiti maamuzi
Baadhi ya kazi zinahitaji programu kuchagua kati ya vitendo
tofauti kulingana na sharti fulani. Katika usimbaji, hili hujulikana kama
uamuzi au uchaguzi. Rejea kazi zifuatazo katika mchezo.
(a) Ikiwa kihusika kitagusa ukingo wa jukwaa, badilisha rangi
yake.
(b) Ikiwa namba ni shufwa, sema Namba ni shufwa, la sivyo
sema Namba ni witiri.
Kazi hizi zote zinahitaji programu kufanya maamuzi. Katika
kazi ya kwanza, programu ina chaguo moja, kubadilisha rangi ikiwa ukingo utaguswa.
Katika kazi ya pili, programu ina chaguzi mbili, kusema Namba ni shufwa au
Namba ni witiri. Ili kufanya maamuzi rahisi katika Scratch, bloku ya ikiwa ()
basi inatumika. Vivyo hivyo, ili kuchagua kati ya chaguzi mbili, bloku ya ikiwa
() basi isivyo inatumika.
Kielelezo: Bloku za ikiwa () basi na ikiwa (
)basi () isivyo lli programu iweze kufanya uamuzi, inahitaji taarifa ya awali.
Taarifa hii inajulikana kama sharti-kwa ajili ya muundo wa udhibiti wa maamuzi,
na huwekwa kwenye umbo la pembe sita lililopo juu ya bloku la maamuzi.
Kuchora maumbo kwenye Scratch
Maumbo ni miongoni mwa vitu
vinavyotumika kuunda michezo rahis inayoshirikisha. Ili kuchora umbo katika
Scratch, unapaswa kuongeza kiendelezi cha Kalamu. Kuongeza kiendelezi cha
Kalamu, fuata hatua zifuatazo:
1. Bofya ikoni ya Ongeza kiendelezi
iliypo kona ya chini kushoto. Angalia Kielelezo (a).
2. Bofya kiendelezi cha Kalamu ili
kuongeza kwenye jalada lako la programu. Angalia Kielelezo (b).
Kielelezo: kuendeleza kiendelezi cha kalamu
Mifano ya bloku ya kiendelzi cha kalamu ni:
![[PDF] Nukuu za somo sayansi darasa la tano free download [PDF] Nukuu za somo sayansi darasa la tano free download](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgzovIoFDx-rsQKsrpKPc5FVKtlrvX380lNGv0HgUq3rZYf8H93Ud0cp13ZncLnp5zGRo8e5g2L1mfScnou2gsnpdpOq3iE5fEw36WJWRmJmPkYvO84gXWglC6SUAXmTI4ipqpj8w_f3Umik60DV9FMJjUqZECoeVu_Xf-2c-uPq3gLtY88nJpMoJe_Qizn/w320-h180-rw/1000025191.jpg)