SURA YA KWANZA.
MAZINGIRA
Mazingira hujumuisha vitu vyote vinavyotuzunguka, vikiwemo viumbe hai na vitu visivyo hai. Viumbe hai ni pamoja na wanyama, mimea na wadudu. Vitu visivyo hai ni pamoja na mchanga, mawe, hewa na maji.
Usalama wa mazingira
Mazingira salama kwa viumbe hai ni yale ambayo hayajaathiriwa kutoka katika uhalisia wake. Mazingira hayo hufanya viumbe hai waishi na kukua vizuri. Mazingira yasiyo salama kwa viumbe hai ni yale yaliyoathiriwa kutoka katika uhalisia wake. Mazingira hayo huathiri afya na ukuaji wa viumbe hai.
Mfano wa mazingira yanayofaa kwa ukuaji wa viumbe hai ni udongo, maji ya mito, maziwa na bahari. Halikadhalika hewa pia ni muhimu kwa viumbe hai. Mazingira hayo yakiathiriwa huwa sio salama kwa viumbe hai.
Uharibifu wa udongo
Soma habari ifuatayo kwa makini, kisha fanya zoezi la 1.
Siku moja mwalimu wa Shule ya Msingi Kidete aliwapa kazi wanafunzi. Kazi hiyo ilikuwa ni kufanya uchunguzi kuhusu vitendo vinavyosababisha uharibifu wa udongo katika mazingira yanayowazunguka. Wanafunzi waliandaa daftari pamoja na kaiamu kwa ajili ya kuandika matokeo ya uchunguzi. Mwalimu aliwasisitiza wanafunzi kuwasilisha kazi zao mara baada ya kumaliza uchunguzi. Baada ya kuwasilisha kazi, mwalimu alimchagua Shukrani na kufanya naye mazungumzo darasani. Mazungumzo hayo yalikuwa kama ifuatavyo:
Mwalimu: Katika uchunguzi ulioufanya, ulibaini vitendo gani vinavyohatarisha usalama wa udongo?
Shukrani: Nilibaini kuwepo kwa utupaji na uchomaji ovyo wa takatak
Mwalimu: Sawa Shukrani, vitu gani ambavyo uliviona vimetupwa, ukagundua vinasababisha uharibifu wa udongo?
Shukrani: Niliona mifuko ya plastiki, makopo, chupa za plastiki na misumari. Vitu vingine ni nyembe, vipande vya bati na vipande vya chupa. Vitu hivi vilikuwa vimezagaa ovyo kila mahali.
Mwalimu: Vitu hivyo unadhani vina madhara gani kwa viumbe hai?
Shukrani: Vitu hivyo huathiri afya za wanyama na mimea. Pia, husababisha kuwepo kwa mazalio ya vijidudu vya magonjwa kama vile malaria. Vilevile, husababisha maambukizi na kuenea kwa magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu na homa ya matumbo.
Mwalimu: Vizuri sana. Nini kifanyike ili kuondoa tatizo hilo?
Shukrani: lnatubidi kukusanya takataka na kuziweka
kwenye
pipa kisha kuzitupa mahali salama au kuzichoma.
Pia, kuchimba shimo na kufukia takataka zinazooza.
Mwalimu: Ni sehemu gani salama ya kuchoma takataka zilizokusanywa?
Shukrani: Ni kwenye shimo la takataka au tanuru maalum.
Mwalimu : Sawa Shukrani, njia salama ni kuzichoma takataka. Lakini moshi wake ni hatari kwa afya., hivyo zichomwe mbali na makazi ya watu. Je, unafikiri takataka gani nyingine zinaweza kuharibu udongo?
Shukrani: Uchafu unaotoka kwenye makazi ya watu kama maji machafu na majitaka yanayotoka vyooni ambayo hutiririka ovyo.
Mwalimu: Kweli kabisa, vilevile umwagaji wa mafuta yanayotoka kwenye magari, mitambo na vifaa mbalimbali huharibu udongo.
Shukrani: Asante sana mwalimu, ninaahidi kuwa balozi wa mazingira.
Mwalimu: Asante sana Shukrani. Naamini, wewe pamoja na wenzako mtakuwa mabalozi mazuri wa mazingira. Mazingira salama, ukiwemo udongo ni makazi ya wadudu wanaosaidia mmeng’enyo wa virutubisho vya mimea katika ardhi. Hivyo, hatuna budi kuutunza.
Kielelezo namba 1. Uchafuzi wa udongo
![]() |
Uchafuzi wa maji
Ukichunguza maeneo unayoishi, kung baadhi ya watu hutupa takataka katika mikondo ya maji. Pia, watu hutiririsha majitaka kutoka vyooni, viwandani na migodini kuelekea kwenye vyanzo vya maji. Maji yanayotoka viwandani na migodini yanaweza kuwa na kemikali zenye sum. Utiririshaji wa majitaka husababisha uchafuzi wa mazingira na vyanzo vya maji.
Aidha, shughuli za kila siku za binadamu huweza kuchafua vyanzo vya maji. Shughuli hizo ni kama kufua, kuoga, kujisaidia ovyo na kulima kandokando ya vyanzo vya maji. Vilevile, wanyama wanapotumia mito, mabwawa na maziwa huchafua maji. Uchafuzi wa vyanzo vya maji husababisha madhara kwa binadamu na viumbe wengine.
Maji yaliyochafuliwa huweza kusababisha magonjwa ya homa ya matumbo, kichocho na kipindupindu. Halikadhalika, maji yaliyochafuliwa kwa kemikali kutoka viwandani, shambani na migodini huweza kusababisha saratani.
Kielelezo namba 2. Uchafuzi wa maji
Uchafuzi wa hewa
Hewa ni mchanganyiko wa gesi mbalimbali zinazopatikana angani. Hewa inaweza ku'iva safi au chafu. Hewa safi ni lie ambayo haina vihatarishi vya afya na mazingira.
Vitu vinavyoweza kuchafua hewa ni vumbi, harufu mbaya, kemikali au vimeiea vya magonjwa. Pia, shughuli mbalimbali za kibinadamu zinachangia katika uchafuzi wa hewa. Shughuli hizo ni kama uchomaji takataka na misitu. Vilevile, moshi wa sumu kutoka viwandani na kwenye magari chakavu huchafua hewa.
Kielelezo namba 3. Uchafuzi wa hewa
Soma habari ifuatayo kwa makini, kisha fanya zoezi la 4.
Siku moja mwalimu wetu alimwalika mtaalamu wa mazingira wa kata ya Mima. Lengo iilikuwa kutueleza athari za uchafuzi wa mazingira. Mtaalamu alieleza kuwa, uchafuzi wa mazingira husababisha vifo vya wanyama na mimea. Vifo hivyo husababishwa na kuchafuka kwa hewa, maji na udongo. Vilevile, utiririshaji wa majitaka kutoka kwenye makazi ya watu na viwandani, huathiri viumbe hai wanaoishi majini.
Aliendelea kusema kuwa, magonjwa kama kichocho na kipindupindu husababishwa na uchafuzi wa mazingira. Magonjwa mengine ni kikohozi, mafua na homa ya matumbo.
Mtaalamu alieleza vitendo vya ukataji miti ovyo husababisha kuongezeka kwa hewa ya kabonidioksidi katika anga. Hewa hii ingetumiwa na mimea kutengeneza chakula na kutoa hewa safi ya oksijeni ambayo hutumiwa na viumbe hai.
Wanafunzi walimuuliza mtaalamu kuhusu madhara ya moshi wa viwandani kwenye mazingira. Mtaalamu alieleza kuwa, moshi wenye sumu huathiri mapafu na kusababisha magonjwa kama vile saratani ya mapafu.
Mtaalamu aliwashukuru wanafunzi kwa kumsikiliza na kuwataka wafanye hadhari iii wasichafue mazingira. Mwalimu alimshukuru mtaalamu kwa ufafanuzi wake mzuri uliowafanya wanafunzi kufurahia somo.
Kutunza mazingira
Ni muhimu kutunza mazingira yetu iii yawe safi na salama. Uchafu wenye takataka mchanganyiko na zisizooza kama mifuko ya plastiki, nyembe na sindano unatakiwa utenganishwe. Pia, vigae vya chupa, sahani na vikombe vichomwe kwenye tanuri au zifukiwe kwenye shimo la Takataka kama mabaki ya chakula, karatasi na majani yaliyopukutishwa na miti zifukiwe kwenye shimo. Baada ya iticpda takataka hizi huoza na kuwa mbolea. Takataka zinazoraa-lkwa urejelezaji zipelekwe viwandani kwa ajili ya kutengeneza vitu vingine.
Kielelezo namba 4. Tanuri
Ni vema majitaka yaelekezwe katika mfumo rasmi wa kutiririsha na kutunza majitaka. Pale ambapo hakuna mfumo huo, maji hayo yahifadhiwe katika mashimo ya majitaka. Mashimo yakijaa majitaka yanyonywe kwa gari maalumu na kupelekwa sehemu zilizotengwa kwa ajili hiyo. Sehemu ambapo hakuna gari maalumu la kunyonyea majitaka, shimo lililojaa lifukiwe na Iichimbwe shimo jingine.
Neema na Musa ni wanafunzi wa Shule ya M.singi Miembeni. Siku moja wakiwa njiani kutoka shuleni, Neema alianzisha mazungumzo kama ifuatavyo:
Neema: Kwa nini tunashauriwa kupanda miti katikamazingira yetu?
Musa: Kwa sababu miti ni muhimu katika maisha yetu yakila siku.
Neema:Je, ni umuhimu gani huo?
Musa: Miti hutupatia kuni, mkaa, hewa ya oksijeni,matunda na kivuli. Halikadhalika, miti hutupatia dawa, mbao na pia ni makazi ya ndege, wanyama na wadudu.
Neema:Asante Musa! Kumbe kuna umuhimu wa kupanda na kutunza miti katika mazingira yetu. Hivi kwa nini watu wanakata miti?
Musa: Watu wanakata miti kwa ajili ya matumizi mbalimbalikama kuni, kuchoma mkaa
na kujengea nyumba.
Neema:Kama watu watakata miti kwa wingi kwa ajili ya kuchoma mkaa nini kitatokea?
Musa: Ukataji wa miti kwa wingi utasababisha kiwango chahewa ya kabonidioksidi kuongezeka. Kuongezeka kwa hewa ya kabonidioksidi kuna madhara kwa viumbe hai na anga. Pia, uchOmaji wa mkaa ukizidi utasababisha jangwa na uchafuzi wa hewa.
Neema:Asante Musa kwa maelezo yako. Je, ni uchomaji wa mkaa pekee ndiyo unaochafua hewa?
Musa: Hapana, vipo vyanzo vingine vinavyochafua hewa.Vyanzo hivyo ni pamoja na vumbi na harufu mbaya kutoka kwenye mifumo ya majitaka iliyoharibika.
Vilevile, moshi kutoka viwandani, magari chakavu na mitambo inayotumia nishati mbalimbali hasa fueli huchafua hewa.
Neema:Nashukuru Musa kwa maelezo yako. Ni vyema tuchukue hatua za kuelimisha jamii iii kudumisha usalama wa hewa.
Musa : Kweli kabisa, jamii ina jukumu la kuhakikishainadumisha usafi na usalama wa hewa. Pia, isichome misitu, ipunguze uchomaji wa mkaa na itumie nishati mbadala kama gesi na umeme.
SURA YA PILI
NISHATI
Nishati ya umeme
Umeme ni nini?
- Umeme ni nishati inayotokana na vyanzo mbalimbali vikiwemo jua, upepo, maji na fueli,
- Vyanzo hivyo huzalisha umeme kwa kutumia mitambo mbalimbali kama paneli za jua na kinuupepo. Pia, hutumia vifaa kama jenereta, dainamo, selikavu na betri.
Kuzalisha umeme kwa kutumia maji
- Nguvu ya maji inayotokana na maporomoko hutumika kuzalisha umeme.
- Tabaini zilizounganishwa kwenye jenereta huzungusha maji kwa kasi. Tabaini ni mashine inayozungushwa na msukumo wa maji.
- Kitendo hiki kinapoendelea umeme huzalishwa. Hapa Tanzania, maporomoko ya maji yanayozalisha umeme yanapatikana Kidatu (Morogoro) na Mtera (Iringa).
- Sehemu nyingine ni Bwawa la Nyumba ya Mungu (Kilimanjaro), Kihansi (Mororogo), Pangani na Hale (Tanga).
Kuzalisha umeme kwa kutumia jua
- Jua lina uwezo wa kuzalisha umeme. Miale ya jua hukusanywa na kifaa maalumu kinachoitwa paneli ya sola.
- Paneli ya sola hubadilisha nishati ya mwanga wa jua kuwa nishati ya umeme. Paneli hizo huweza kuunganishwa na betri na kutunza umeme kwa matumizi mbalimbali.
Kielelezo Namba 1. Paneli ya solar.
Kuzalisha umeme kwa kutumia upepo
- Umeme pia huweza kuzalishwa kwa kutumia upepo. Upepo unapovuma, mabapa ya kinuupepo huzungushwa.
- Kinuupepo ni mashine ya kufua umeme inayotumia msukumo wa upepo. Kasi ya upepo husababisha jenereta Iililounganishwa na kinuupepo kuzalisha umeme.
- Mpaka sasa, mitambo ya kuzalisha umeme huu kwa wingi katika nchi ya Tanzania inapatikana katika mkoa wa Singida.
Kielelezo Namba 2. Nishati ya Upepo.
Kuzalisha umeme kwa kutumia fueli
- Fueli hutoa nishati ya joto ambayo hubadilishwa na kuwa nishati ya umeme.
- Fueli hizo ni dizeli, petroli, makaa ya mawe na gesi asilia. Vifaa kama jenereta hutumia nishati hizo kuzalisha umeme.
- Kuna mitambo inayozalisha umeme mkubwa kwa kutumia dizeli. Mitambo hiyo ipo Ubungo Dar es Salaam na Dodoma.
- Pia, mitambo mingine ya dizeli huzalisha umeme mdogo unaotumika shuleni, zahanati, makanisani na misikitini.
Kielelezo Namba 3. Mitambo ya gesi Mtwara.
- Mitambo ya gesi asilia hupatikana Mtwara na Kinyerezi I na Kinyerezi II jijini Dar es Salaam.
- Umeme unaotengenezwa na vyanzo mbalimbali hutiririka kupitia njia maalumu. Njia hiyo imeundwa na chanzo cha umeme, waya, swichi, na kifaa kinachotumia umeme.
- Muunganiko wa vifaa hivi ambavyo umeme hupitia huitwa sakiti. Umeme hutiririka ikiwa sakiti imekamilika.
- Kama umeme hautiririki inaashiria kutokamilika kwa sakiti. Umeme hautiririki kwenye sakiti endapo waya umekatika au swichi imezimwa.
Mabadiliko ya nishati ya umeme
- Nishati ya umeme inaweza kubadilishwa kutoka nishati moja kwenda nyingine kutegemea kifaa kilichotumika.
- Kwa mfano, kurunzi hutumia nishati ya umeme kutoka kwenye selikavu na kutoa nishati ya mwaga na joto.
Matumizi ya nishati ya umeme
Soma habari hii kwa makini
- Siku moja, Rehema na wanafunzi wenzake walikuwa wakitoka shuleni. Walipokuwa njiani, waliona gall kubwa Iffilokuwa limesimama karibu na ofisi ya Mtendaji Kata. Nje ya ofisi hiyo walionekana vijana wengi wakishangilia.
- Vijana wawili walielekea kwenye miango wa gari hilo na kuufungua. Walishusha makasha mengi na kuyapeleka katika ofisi ya Mtendaji Kata. Rehema na wenzake walisogea karibu ili waone makasha hayo yalikuwa na nini.
- Waligundua kuwa ndani ya makasha kulikuwa na vifaa mbalimbali vya umeme. Vifaa hivyo vilikuwa betri, nyaya za umeme, soketi na paneli za sola.
- Rehema na wenzake waliamua wasiondoke bila kujua kazi ya vitu hivyo. Mtendaji Kata aliwaambia kuwa, ni vifaa vitakavyotumika kuunganishia umeme unaotokana na nishati ya jua. Hivyo, muda si mrefu kutakuwa na umeme unaotumia mionzi ya jua kijijini kwao.
- Baada ya wiki moja nyumba nyingi zilikuwa zimewekewa vifaa maalumu vinavyojulikana kama paneli za sola. Wananchi katika !qui hicho walianza kutumia umeme unaotokana na mionzi ya jua kwa shughuli mbalimbali. Rehema alifurahi kwanialiweza kutumia nishati ya umeme kwa kazi mbalirnbali za nyumbani. Vilevile, Rehema aliweza kujisomea wakati wa usiku, kusikiliza redio, na kuangalia runinga.
- Halikadhalika, Rehema aliweza kunyoosha nguo zake kwa kutumia pasi ya umeme kwa haraka na kuwahi shuleni.
- Siku moja Rehema alimuomba mwalimu awaeleze wenzake jinsi chao kilivyofaidika na umeme. Mwalimu alimpa nafasi naye akawaeleza kuwa, umeme hutumika kwenye jiko kwa ajili ya kupikia.
- Vilevile, hutumika katika jokofu iii kuhifadhi vyakula na kwenye mashine za kutengenezea vinywaji. Halikadhalika, hutumika kwenye pampu za kusukumia maji na mashine za kunyolea nywele.
- Mwalimu aliongezea kueleza kuwa, umeme hutumiwa kuchomelea vyuma na kuendeshea mitambo viwandani. Hivyo, nishati ya umeme husaidia kutoa ajira kwa watu.
- Umeme ni rafiki unapotumiwa kwa kuzingatia kanuni na masharti. Hata hivyo, mwalimu aliwaeleza wanafunzi kuwa, hitilafu ya umeme husababisha moto, mlipuko na hata kifo. Wanafunzi walimshukuru mwalimu na Rehema kwa kutoa elimu kuhusu matumizi ya umeme.
Nishati ya mwanga
- Nishati ya mwanga inaweza kuonekana kutoka kwenye vyanzo mbalimbali kama vile jua. Pia, huweza kutokea kwa kubadilisha nishati moja kwenda nishati nyingine.
- Mfano nishati ya umeme hubadilishwa iii kupata nishati ya mwanga. Nishati hii huweza kuonekana inapokutana na vitu mbalimbali vinavyoruhusu na visivyoruhusu mwanga kupenya.
Vitu vinavyoruhusu na visivyoruhusu mwanga kupenya
- Baadhi ya vitu vinaruhusu miale ya mwanga kupenya. Pia, vipo vitu visivyoruhusu miale ya mwanga kupenya.
Kielelezo Namba 4 kupenyeza kwa mwanga
- Vitu vinavyoruhusu miale ya mwanga kupenya huitwa angavu, mfano kioo na gilasi. Vile visivyoruhusu miale ya mwanga kupenya huitwa vikinza nuru, mfano ubao, kitabu na ukuta.
Kutokea kwa vivuli
- Kivuli ni sehemu yenye giza inayoonekana upande wa pili wa kitu kisichopitisha mwanga. Pia, umbo Ia kivuli huonekana kushabihiana na kitu kilichozuia mwanga kupenya.
Kielelezo Namba 5 kivuli
Soma habari ifuatayo kwa makini
Mwajuma na wenzake wanasoma darasa la nne katika Shule ya Msingi Shaurimoyo. Siku moja mwalimu wa somo Ia Sayansi aliwafundisha wanafunzi tabia za mwanga. Aliwaeleza kuwa tabia mojawapo ya mwanga ni kusafiri katika mstari mnyoofu. Vilevile, mwanga ukitua kwenye baadhi ya vitu vigumu huzuiwa na kutengeneza kivuli.
Mwalimu akawaambia, "Ninataka mfanye zoezi muone mwanga unapozuiwa nini kitakachotokea?" Mwalimu aliwaeleza, "Wakati wa asubuhi, jua likiwa linachomoza, simama sehemu ya wazi. Hakikisha jua linakumulika mgongoni na angalia nini kinatokea mbele yako. Pia, shika mpira mkononi, kisha nyoosha mkono wako upande wa jua na angalia chini. Kwa kutumia vitu mbalimbali, fanya vitendo hivyo na kuangalia matokeo yake."
Siku iliyofuata baada ya jua kuchomoza, Mwajuma na wenzake walielekea uwanjani iii kufanya uchunguzi. Walisimama kama walivyoelekezwa na mwalimu. Wakaona maumbo yenye giza mbele yao kama inavyoonekana kwenye kielelezo namba 12. Waliandika walichokiona na kuelekea darasani kuendelea na masomo.
Mwalimualiwauliza walichogundua baadaya kufanya uchunguzi. Mwanafunzi mmoja anayeitwa Kalunde alijibu, "Nimeona umbo jeusi ardhini mbele yangu." Mwajuma aliongezea kwa kusema, "Mimi niliona umbo linaloshabihiana na umbo langu." Mwanafunzi mwingine aliongeza, "Mimi niliona umbo langu pamoja na umbo la mpira."
Baada ya hapo mwalimu alieleza, "Hicho mlichokiona kinaitwa kivuli." Kivuli hutokea mwanga unapotua na kuzuiwa na kitu kisicho angavu. Kwa hiyo, kivuli ni matokeo ya kuzuiwa kwa mwanga kusafiri katika mstari ulionyooka. Aidha, kivuli hubadili uelekeo na ukubwa kadiri chanzo cha mwanga kinavyobadili uelekeo. Mwajuma na wenzake walifurahia somo kwa kuwa waligundua namna kivuli kinavyotokea.
Kuakisiwa kwa miale ya mwanga
Kielelezo Namba 6 kuakisi kwa mwanga
Kuakisiwa kwa mwanga ni kitendo cha kurudishwa kwa miale ya mwanga inapotua kwenye sura nyororo na inayong'aa. Mfano wa kifaa chenye sura nyororo na inayong'aa ni kioo bapa.
Miale ya mwanga inapotua katika nyuso nyororo zinazong'aa huakisiwa. Kuakisiwa kwa miale ya mwanga husababisha kutengenezwa kwa taswira mbalimbali katika nyuso hizo.
Kupinda kwa miale ya mwanga
Miale ya mwanga hupinda inapotoka midia moja kwenda midia nyingine angavu. Mfano, kutoka kwenye midia ya hewa kwenda midia ya maji. Hatuoni miale ya mwanga ikipinda bali tunaona matokeo ya kupinda kwa miale ya mwanga.
Kielelezo Namba 7 kupinda kwa mwanga.