Visit Website

Kwa mahitaji ya mitihani, Maazimio ya kazi, Shajara, Notes, na materials mbalimbali ya kielimu, wasiliana nasi ujipatie huduma zetu kwa gharama nafuu sana.

Tunatoa huduma za materials mbalimbali za kielimu kwa gharama nafuu wasiliana nasi leo..

Nukuu za Somo Sayansi Darasa la Tano Mtaala Mpya 2026 PDF Download

Nukuu za Somo Sayansi | Darasa la Tano | Mtaala Mpya 2026 | PDF Download
[PDF] Nukuu za somo sayansi darasa la tano free download

NOTES ZA SAYANSI DARASA LA TANO 2026

Mtaala Mpya wa Mwaka 2026

MADA ZA SAYANSI DARASA LA 5 MTAALA MPYA

Sura ya Kwanza: Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula

  • Dhana ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula

  • Sehemu za mfumo wa mmeng'enyo wa chakula

  • Kasoro katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula

  • Tabia sahihi za ulaji wa chakula

Sura ya Pili: Ukuaji katika mimea na wanyama

  • Dhana ya ukuaji katika mimea na wanyama

  • Ukuaji katika mimea

  • Mahitaji muhimu katika ukuaji wa mimea

  • Ukuaji katika wanyama

  • Hatua za ukuaji katika mwili wa binadamu

  • Njia za kuhimili mabadiliko yanayotokea wakati wa balehe

Sura ya Tatu: Mfumo wa uzazi

  • Dhana ya mfumo wa uzazi wa binadamu

  • Mfumo wa uzazi wa binadamu

  • Kasoro katika mfumo wa uzazi

  • Utunzaji wa mfumo wa uzazi

Sura ya Nne: Usumaku

  • Dhana ya usumaku...

  • Maumbo ya sumaku

  • Sifa za sumaku

  • Matumizi ya sumaku

  • Utunzaji wa sumaku

  • Msamiati

Sura ya Tano: Usimbaji katika kompyuta

  • Muundo wa kudhibiti mlolongo

  • Vibadilika na opereta

  • Muundo wa kudhibiti maamuzi

  • Kuchora maumbo kwenye Scratch



                                                                

SURA YA KWANZA: MFUMO WA MMENG’ENYO WA CHAKULA

Dhana ya mfumo wa mmeng’enyo wa chakula

Mmeng'enyo wa chakula ni mchakato wa kibaiolojia ambapo chakula huvunjwavunjwa kuwa chembechembe ndogo zenye virutubisho ambavyo mwili unaweza kufyonza. Virutubisho hivi hutumiwa na mwili kwa ajili ya kupata nishati, ukuaji, matengenezo ya tishu zilizoharibika na ulinzi wa mwili dhidi ya magonjwa. Ili mwili uweze kupata virutubisho hivi, chakula lazima kivunjwevunjwe kuwa chembechembe ndogo zinazoweza kufyonzwa na kutumiwa na mwili. Mmeng'enyo wa chakula hufanyika katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.

Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ni mkusanyiko wa ogani au viungo vya mwili wa binadamu vinavyohusika na kuvunjavunja chakula kuwa chembechembe ndogo zenye virutubisho zinazoweza kufyonzwa na kutumiwa na mwili. Ili kudumisha afya ya mfumo huu, ni muhimu kula mlo kamili kwa wakati sahihi, kunywa maji ya kutosha, kuepuka kula vyakula vyenye mafuta au sukari kwa wingi ili kuimarisha afya ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. Mbali na binadamu, wanyama wengine pia wana mifumo ya kumeng'enyachakula inayotofautiana kutokana na aina ya vyakula wanavyokula.

Sehemu za mfumo wa mmeng’enyo wa chakula

Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula unahusisha ogani mbalimbali ambazo hufanya kazi kwa pamoja ili kurahisisha uvunjwaji wa chakula. Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula wa binadamu huanzia kwenye kinywa hadi kwenye njia ya haja kubwa. Mfumo huu unajumuisha njia ya chakula, ogani na tezi zinazofanya kazi pamoja. Sehemu kuu za njia ya chakula ni kinywa, koromeo, umio, mfuko wa tumbo, utumbo mwembamba, na utumbo mpana kama inavyoonekana kwenye Kielelezo. Utumbo mwembamba unajumuisha duodeni na iliamu. Vilevile, utumbo mpana unajumuisha koloni, puru na njia ya kutolea haja kubwa. Ogani zinazounda mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ni pamoja na ulimi, ini, kongosho, na kibofu nyongo. Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula pia unajumuisha tezi za mate na zile zinazopatikana katika mfuko wa tumbo. Vilevile, baadhi ya ogani kama ini, kongosho na kibofu nyongo zina tezi zinazozalishavimeng'enya vinavyotumika katika kumeng'enya chakula.

Kielelezo: mfumo wa mmeng’enyo wa chakula wa binadamu

 

Kinywa

Mchakato wa mmeng'enyo wa chakula huanzia kinywani, ambako chakula hutafunwa na kuvunjwavunjwa na meno. Pia, katika sehemu hii, vyakula huchanganywa na mate. Vyakula vyenye wanga huanza kumeng'enywa katika sehemu hii na kisha kusafirishwa kupitia umio hadi mfuko wa tumbo.

 

Koromeo

Ni sehemu ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula inayopatikana kati ya kinywa na umio. Kazi yake ni kuongoza chakula kutoka kinywani hadi kwenye umio. Chakula huzuiwa kuingia kwenye njia ya hewa kwa kutumia kifuniko kinachofunga njia ya hewa wakati wa kumeza chakula. Kifuniko hicho huitwa kidakatonge.

 

Umio

Umio ni bomba lenye misuli linalounganisha koromeo na sehemu ya juu ya mfuko wa tumbo. Chakula husafiri kupitia umio kutokana na mfululizo wa ukazaji na ulegezaji wa misuli ya kuta za umio. Hali hiyo huifanya misuli ya kuta za umio kusukuma chakula kuingia katika mfuko wa tumbo.

 

Mfuko wa tumbo

Ndani ya mfuko wa tumbo, chakula huchakatwa zaidi kwa msaada wa asidi na vimeng'enya. Asidi na vimeng'enya hivi husaidia kumeng'enya protini, wanga na mafuta, na kubadilisha chakula kuwa mchanganyiko mzito unaoitwa chime. Kisha, mchanganyiko huo husafirishwa Kwenda kwenye utumbo mdogo ili kumeng'enywa zaidi na kuruhusu ufyonzwaji wa virutubisho.

 

Utumbo mwembamba

Sehemu hii inapatikana kati ya mfuko wa tumbo na utumbo mpana. Sehemu ya mwanzo ya utumbo mwembamba huitwa duodeni. Duodeni hupokea vimeng'enya kutoka kwenye kongosho na nyongo kutoka kwenye kibofu nyongo kwa ajili ya kuvunjavunja chakula. Mmeng'enyo wa chakula vyenye wanga, protini na mafuta hufanyika katika sehemu hii. Sehemu ya mwisho ya utumbo mwembamba huitwa iliamu. Mchakato wa mmeng'enyo wa vyakula vyenye wanga huishia katika iliamu. Chakula kinapofika kwenye iliamu, kinachochea ukuta wa iliamu kutoa majimaji. Majimaji haya yana vimeng'enya ambavyo huendelea kumalizia mmeng'enyo wa protini, wanga na mafuta. Kazi ya utumbo mwembamba ni kufyonza virutubisho kutoka kwenye chakula kilichomeng'enywa ili viweze kutumika katika kazi mbalimbali mwilini.

 

 

Utumbo mpana

Utumbo mpana unapatikana baada ya utumbo mwembamba. Kazi yake ni kufyonza maji na madini kutoka kwenye mabaki ya chakula na kuyarejesha mwilini. Pia, kutumia mabaki ya chakula kutengeneza kinyesi kwa ajili ya kutolewa nje ya mwili. Vilevile, utumbo mpana una bakteria wenye manufaa wanaosaidia kumeng'enya mabaki ya chakula na kutengeneza baadhi ya vitamini. Koloni, puru na njia ya kutolea haja kubwa ni sehemu za utumbo mpana.

 

Koloni

Sehemu ya kwanza ya utumbo mpana inaitwa koloni. Sehemu hii hutumika kurejesha maji mwilini kutoka kwenye chakula kilichovunjwavunjwa. Pia, ni mahali ambapo baadhi ya virutubisho kama vitamini hutengenezwa na bakteria wanaopatikana katika sehemu hii. Koloni hutumika pia katika kuhifadhi kinyesi kabla ya kutolewa nje ya mwili.

 

Puru

Ni sehemu ya pili ya utumbo mpana ambapo kinyesi huhifadhiwa kwa muda kabla ya kutolewa nje ya mwili kama haja kubwa. Sehemu hii hudhibiti uondoaji wa kinyesi kutoka mwilini.

 

Njia ya kutolea haja kubwa

Hii ni sehemu ya mwisho ya utumbo mpana ambayo hutumika kutolea kinyesi. Kinyesi hutolewa nje ya mwili kupitia njia ya kutolea haja kubwa.

Kinyesi ni mabaki ya chakula ambayo hayakumeng'enywa na kufyonzwa na mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.

 

 

Kasoro katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula

Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula unaweza kuathiriwa na kasoro mbalimbali zinazoweza kupunguza ufanisi wa uvunjaji-vunjaji wa chakula au ufyonywaji wa virutubisho. Kasoro katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ni hali inayoathiri utendaji kazi wa kawaida wa mfumo wa mmeng'enyo wa chakula na kufanya iwe vigumu kwa mwili kumudu kumeng'enya na kufyonza chakula ipasavyo. Kasoro hizo zinaweza kuwa za kimaumbile, kurithi au zinazotokana na mtindo wa maisha na lishe duni. Baadhi ya kasoro za mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ni kama zifuatazo:

 

Kupata choo kigumu

Hii ni kasoro katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula inayosababisha ugumu wa kupitisha kinyesi au kuwa na kinyesi kigumu na kikavu. Kasoro hii husababishwa na ulaji wa vyakula vyenye kiwango cha chini cha nyuzinyuzi, kutokunywa maji ya kutosha na ukosefu wa mazoezi ya mwili. Pia, matatizo ya kiafya kama vile utendaji duni wa utumbo mpana husababisha kupata choo kigumu.

 

Njia za kuzuia

Hali hii huzuiawa kwa kula vyakula vyenye nyuzinyuzi za kutosha kama vile matunda na mbogamboga, kunywa maji ya kutosha na kufanya mazoezi mara kwa mara.

 

Kuvimbiwa

Ni hali ambayo mfuko wa tumbo hujaa, kuwa mgumu au kuvimba, mara nyingi hutokana na mkusanyiko wa gesi katika mfuko wa tumbo. Tatizo la kuvimbiwa husababishwa na kula chakula kingi kupita kiasi, kula vyakula vinavyosababisha gesi au tumbo kutovumilia baadhi ya vyakula. Dalili za mtu aliyevimbiwa ni kuumwa tumbo, kuhisi tumbo kujaa gesi na kupiga mbweu. Wakati mwingine gesi hiyo huwa na harufu kali na mbaya.

Njia za kuzuia

Ili kuzuia kuvimbiwa unapaswa kula chakula kwa kiasi na kutafuna polepole ili kupunguza kiasi cha hewa inayomezwa. Vilevile, kunywa maji ya kutosha ili kurahisisha mmeng'enyo wa chakula katika mfuko wa tumbo. Kupunguza ulaji wa vyakula vyenye gesi kama vile maharagwe na unyweji wa vinywaji vyenye gesi kama vile soda. Pia, ulaji wa matunda na mboga za majani huzuia kuvimbiwa.

 

Kiungulia

Hii ni hali inayojitokeza wakati asidi kutoka kwenye mfuko wa tumbo inapopanda hadi kwenye umio na kusababisha maumivu au muwasho katika koo. Dalili za kiungulia ni pamoja na kuhisi maumivu ya kuungua kifuani. Pia, kucheua sana na kuhisi uchachu mdomoni. Kiungulia husababishwa na kula chakula kingi kupita kiasi. Pia, husababishwa na kula vyakula vyenye viungo vingi au vyenye mafuta mengi. Vyakula hivi huchukua muda mrefu zaidi kumeng'enywa na vinaweza kuongeza uzalishaji wa asidi tumboni. Sababu nyingine ya kiungulia ni kula vyakula vyenye asidi kama limau na ndimu kwa wingi. Vinywaji kama vile soda, kahawa na pombe vinaweza kusababisha kiungulia. Pia, kula chakula muda mfupi kabla ya kwenda kulala kunaweza kusababisha kiungulia.

 

Njia za kuzuia

Unaweza kuzuia kiungulia kwa kula chakula taratibu ili kurahisisha mmeng'enyo wa chakula. Pia, kula chakula kidogokidogo lakini mara kwa mara. Njia nyingine ni kupunguza ulaji wa vyakula vinavyosababisha kiungulia kama vile chungwa, limao, chenza, viazi, maharagwe na nyanya. Pia, viungo na mafuta mengi ni miongoni mwa vyakula vinavyotakiwa kuepukwa. Epuka kulala mara tu baada ya kumaliza kula. Vilevile, epuka kufanya mazoezi au kazi ngumu muda mfupi baada ya kula chakula. Hali ya kiungulia ikizidi ni vyema kupata ushauri wa kitabibu.

 

 

Vidonda vya tumbo

Hali hii hutokana na kuchubuka kwa utando wa ute kwenye ukuta wa mfuko wa tumbo. Michubuko hiyo husababishwa na ulaji wa vyakula vyenye asidi na kukaa na njaa kwa muda mrefu. Pia, maambukizi ya bakteria husababisha michubuko katika kuta za mfuko wa tumbo. Asidi iliyoko kwenye mfuko wa tumbo huunguza kuta zenye michubuko na kutengeneza vidonda. Vidonda vya tumbo huleta maumivu makali tumboni. Mara nyingi vidonda vya tumbo vikiwa vikubwa huvuja damu. Dalili za vidonda vya tumbo ni pamoja na maumivu makali kama ya kuungua kwenye mfuko wa tumbo. Dalili nyingine ni kutapika damu na kupata haja kubwa iliyochanganyika na damu.

 

Njia za kuzuia

Unaweza kuepuka vidonda vya tumbo kwa kula kwa wakati na kupunguza

ulaji wa vyakula vyenye asidi nyingi. Vilevile, kuacha kuvuta sigara,

kunywa pombe au vinywaji vikali husaidia kuzuia vidonda vya tumbo.

 

Tabia sahihi za ulaji wa chakula

Tabia sahihi za ulaji wa chakula ni muhimu ili kudumisha afya bora na kuzuia matatizo yanayoweza kujitokeza katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. Ulaji sahihi unajumuisha mlo kamili wenye makundi yote ya vyakula kwa uwiano unaofaa. Makundi haya ya vyakula hujumuisha wanga, protini, mafuta, vitamini, madini na maji. Pia, ni muhimu kuwa na muda maalumu wa kula na kupunguza kukaa muda mrefu bila kula au kula vyakula visivyo na virutubisho vya msingi. Tunashauriwa kula vyakula vya nafaka zisizokobolewa na kunywa maji ya kutosha ili kuuwezesha mfumo wa mmeng'enyo wa chakula kufanya kazi kwa ufanisi. Ni vema kunywa maji nusu saa kabla au baada ya kula ili kuboresha mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. Ukizingatia tabia hizi, utaboresha afya ya mwili na kujikinga dhidi ya matatizo kwenye mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.

SURA YA PILI: UKUAJI KATIKA MIMEA NA WANYAMA

Dhana ya ukuaji katika mime ana Wanyama

Ukuaji katika mimea na wanyama ni mchakato unaojumuisha kuongezeka au kubadilika kwa ukubwa wa maumbile, yaani urefu, upana, pamoja na uzito. Ukuaji ni mabadiliko ya kudumu usioweza kubadilishwa. Mabadiliko haya, hutokea kutokana na kurefuka na kuongezeka kwa idadi za seli na mgawanyiko wa seli katika kufanya kazi fulani. Mimea hukua kwa kuongeza urefu wa ncha za mizizi na shina. Pia, mmea hukua kwa kuongezeka kwa mzingo wa shina. Vivyo hivyo, wanyama hukua kwa kuongezeka kwa urefu na uzito wa miili yao.

Ukuaji wa mimea na wanyama hupitia hatua mbalimbali za mabadiliko. Kwa mimea, mabadiliko yanahusisha kuota kwa mbegu, kutokea kwa majani, mizizi na sehemu nyingine kama vile maua, na mbegu au matunda.

Kwa upande wa wanyama, mabadiliko hujumuisha mabadiliko ya umbo la mwili na tabia. Mfano wa mabadiliko kwa wanyama ni buu kubadilika na kuwa kipepeo na mtoto kukua na kuwa mtu mzima. Mabadiliko katika mimea na wanyama yanahusisha mabadiliko ya kimwili na kitabia ambayo ni muhimu kwa maisha ya mmea au mnyama.

 

Ukuaji katika mimea

Hatua za ukuaji wa mmea ni mfululizo wa mabadiliko yanayotokea katika vipindi mbalimbali vya maisha ya mmea kuanzia kuota kwa mbegu hadi kufa kwake. Kila hatua ina mabadiliko yanayosaidia mmea kukua na kuendelea na mzunguko wa maisha yake. Hatua hizo ni kuota kwa mbegu, hatua ya mche, ukuaji wa majani, hatua ya uzazi na hatua ya uzee.

Kielelezo: hatua za ukuaji wa mmea

(a) Hatua ya kuota kwa mbegu

Mbegu iliyokomaa huanza kuota pale inapopata mahitaji muhimu ya uotaji ambayo ni mwanga wa jua, maji, hewa, virutubisho na jotoridi linalostahili. Katika hatua hii, mizizi huanza kutoka katika kitungamizizi kilichopo kwenye mbegu na kukua kuelekea kwenye udongo. Mizizi hufyonza maji na virutubisho kutoka katika udongo ili kusaidia uotaji. Pia, shina chipukizi huanza kuota kutoka katika kiinishina kilichopo kwenye mbegu na kukua kuelekea juu ya udongo ili kuanza kutengeneza shina na majani. Katika hatua hii chakula kilichohifadhiwa katika mbegu hutumika ili kuipa mbegu nguvu ya kuota.

 

(b) Hatua ya mche

Baada ya kuota kwa mbegu, hatua ya mche hufuata. Katika hatua hii, mche huanza kukua kwa haraka. Idadi ya majani huongezeka, mizizi huendelea kukua na kuimarika ndani ya udongo ili kufyonza maji na virutubisho. Katika hatua hii kiwango cha chakula huwa kidogo, hivyo mche huanza kutengeneza chakula chake chenyewe kupitia usanisinuru.

(c) Hatua ya ukuaji wa majani

Katika hatua hii, mmea huendelea kukua na idadi ya majani huongezeka. Mizizi, shina na matawi huendelea kukua na kuimarika. Mmea huendelea kujitengenezea chakula chake kupitia usanisinuru.

 

(d) Hatua ya uzazi

Hii ni hatua ambayo mmea hukomaa na kubadilika kutoka katika hatua ya ukuaji wa majani hadi hatua ya uzazi. Katika hatua hii, baadhi ya mimea huanza kuotesha machapuo. Machapuo haya huendelea kukua na kuwa maua ambayo yana sehemu za uzazi. Maua huchavushwa na kurutubishwa na kupelekea kuwa matunda au mbegu. Matunda yana mbegu ambazo hutumika kuzalisha mimea mipya. Mimea kama tikitimaji, chungwa, nyanya, parachichi, mahindi, na maharagwe huzalisha matunda yenye mbegu. Hata hivyo, kuna baadhi ya mimea ambayo haitoi maua, lakini huzalisha mbegu zinazoweza kuota na kutengeneza mimea mipya.

 

(e) Hatua ya uzee

Uzee ni mchakato wa asili wa kuzeeka kwa mimea, ambapo mgawanyiko wa seli katika kufanya kazi fulani hukoma. Hii husababisha tishu na ogani za mmea kupoteza uwezo wake wa kufanya kazi polepole hadi kufikia hatua ya kufa. Hatua hii hutokea katika hatua zote za ukuaji wa mmea japokuwa kasi yake huongezeka kwa baadhi ya mimea baada ya kutoa mbegu. Tofauti na mimea ya msimu mmoja, mimea ya muda mrefu uzee hutokea katika ogani kama vile majani na maua. Hii huiruhusu mimea hiyo kuendelea kuishi na kukua kwa miaka mingi hata baada ya ogani hizo kufa na kuondolewa.

 

Mahitaji muhimu katika ukuaji wa mimea

Mimea hukua na kustawi vizuri pale inapopata mahitaji yake muhimu.

Kielelezo: mahitaji muhimu katika ukuaji wa mmea.

Ukuaji wa mmea hutegemea upatikanaji wa mahitaji muhimu ambayo ni mwanga wa jua, hewa, maji, virutubisho na jotoridi stahiki ili kuiwezesha kukua vizuri. Ukosefu wa moja ya mahitaji haya huweza kuathiri ukuaji wa mmea. Kwa mfano, mmea unaweza kupata mwanga wa jua wa kutosha, lakini ukikosa maji au virutubisho vya kutosha, ukuaji huathirika. Yafuatayo ni mahitaji muhimu kwa ukuaji wa mimea:

 

Mwanga wa jua

Mwanga wa jua husaidia mimea kukua vizuri. Jua hutoa nishati ya mwanga na joto. Mimea hutumia nishati ya mwanga kujitengenezea chakula chake. Majani ya mimea yana umbijani ambalo husharabu mwanga wa jua ili kusaidia kutengeneza chakula cha mmea. Mchakato wa mimea kutumia mwanga wa jua, maji na kabonidayoksaidi kutengeneza chakula chake huitwa Usanisinuru. Bila mwanga wa jua wa kutosha, mimea haiwezi kukua vizuri kwa sababu itakosa chakula.

 

 

Hewa

Mimea hutumia gesi ya kabonidayoksaidi katika usanisinuru. Gesi hii huchukuliwa na mimea kupitia matundu yaliyopo kwenye majani yanayoitwa stomata. Stomata hufunguka na kuruhusu gesi ya kabonidayoksaidi kuingia ili kuiwezesha usanisinuru kukamilika. Upungufu wa gesi ya kabonidayoksadi husababisha kupu mimea kujitengenezea chakula chake. Mimea inahitaji oksijeni ambayo hutumika kuunguza chakula na kutengeneza nishati inayohitajika ukuaji wa mimea.

Maji

Maji ni mojawapo kati ya mahitaji muhimu katika ukuaji wa mimea. Mimea huhitaji maji ili iweze kukua vizuri. Vilevile, maji ni mojawapo ya mahitaji muhimu katika usanisinuru. Maji hufyonzwa kutoka kwenye udongo kupitia mizizi. Ncha za mizizi zina vinyweleo vidogo ambavyo husharabu maji kwa njia ya osimosisi. Baada ya maji kufyonzwa huingia katika mzizi, kisha husafirishwa kupitia shina hadi kwenye majani. Umuhimu wa maji katika ukuaji wa mimea ni:

(a) Kuyeyusha virutubisho kwenye udongo ili viweze kufyonzwa na mizizi. Virutubisho husaidia mimea kukua vizuri.

(b) Kusafirisha chakula na kusambaza kutoka kwenye majani Kwenda sehemu zingine za mimea.

(c) Kusawazisha kiwango cha joto katika mimea.

(d) Kufanya mimea kuwa imara.

(e) Kusaidia mimea kujitengenezea chakula chake kupitia usanisinuru.

 

Virutubisho

Mimea inahitaji aina mbalimbali za virutubisho kama vile madini na vitamini ili iweze kukua vizuri. Virutubisho vya msingi kwa ukuaji wa mmea ni pamoja na naitrojeni, fosiforasi na potasiamu. Virutubisho hivi hufyonzwa na mimea kutoka ardhini kupitia mizizi. Mimea hupata virutubisho kutoka kwenye udongo au sehemu nyingine ilipopandwa. Vinyweleo vidogo vilivyopo kwenye ncha za mizizi hufyonza maji na virutubisho kwa njia ya osimosisi. Baada ya kuingia kwenye vinyweleo vya mizizi, virutubisho husafirishwa kupitia mzizi mkuu hadi kwenye shina na hatimaye kufikishwa sehemu mbalimbali za mmea.

 

Jotoridi

Mimea huhitaji jotoridi sahihi ili iweze kukua vizuri. Jotoridi sahihi ni muhimu wakati wa uotaji wa mbegu na usanisinuru. Jotoridi likiwa juu kupita kiasi, mimea hupoteza maji na kukauka. Pia, jotoridi la chini hufanya mimea kushindwa kusanisi chakula chake, mbegu kushindwa kuota na hata kupelekea mimea kufa.

 

UKUAJI KATIKA WANYAMA

Ukuaji wa wanyama hutegemea uwepo wa mahitaji muhimu kama hali ya hewa na mazingira yanayofaa, lishe bora na upatikanaji wa maji ya kutosha.

 

Lishe bora

Wanyama wanahitaji mlo kamili unaojumuisha virutubisho vyote muhimu kama protini, wanga, mafuta, vitamini na madini. Upungufu wa virutubisho hivi katika chakula unaweza kusababisha ukuaji hafifu na maendeleo duni ya mwili.

 

Hali ya hewa na mazingira

Wanyama huathiriwa na mazingira wanamoishi. Hali zisizofaa kama joto kali, baridi kupita kiasi, hewa isiyo safi, na uhaba wa nafasi huweza kusababisha msongo wa mawazo na kupunguza kasi ya ukuaji wao. Ili miili ya wanyama ifanye kazi kwa ufanisi, wanahitaji joto la wastani. Aidha, kiwango sahihi cha mwanga katika mazingira kinahitajika katika ukuaji wa wanyama. Kwa baadhi ya spishi, mwanga wa kutosha huchochea hamu ya kula na uzalishaji wa homoni, hivyo kuongeza kasi ya ukuaji na uzalishaji.

Maji

Wanyama wanahitaji maji safi na salama katika ukuaji wao. Maji ni hitaji muhimu katika shughuli za mwili kama mmeng'enyo wa chakula, udhibiti wa joto la mwili na usafirishaji wa virutubisho ndani ya mwili.mambo haya yote ni muhimu kwa ukuaji wa wanyama. Ifuatayo ni mifano ya mabadiliko mbalimbali katika ukuaji wa wanyama:

(a) Vipepeo hupitia hatua mbalimbali za ukuaji ambazo ni:

(b) chura hupitia hata zifuatazo za ukuaji:

(c) binadamu hupitia hatua zifatazo za ukuaji

Hatua za ukuaji katika mwili wa binadamu

Ukuaji wa mwili wa binadamu umegawanyika katika hatua mbalimbali. Hatua hizo ni utoto wa awali, utoto, ujana utu uzima na uzee. Kila hatua huhusisha mabadiliko mahususi ya kimeumbile.

 

(a) Utoto wa awali

Hii ni hatua ya kwanza ya ukuaji wa binadamu ambayo huanzia pindi mtoto anapozaliwa hadi kufikia miaka miwili. Hiki ni kipindi ambacho mtoto amezaliwa na anaanza kujifunza vitu mbalimbali. Katika kipindi hiki mtoto hujifunza kugusa, kutembea na kuwa na hisia. Kadri muda unavyoenda mtoto huanza kushika kichwa, kukaa chini, kutambaa, kujizungusha na kutembea kwa hatua chache bila msaada. Baada ya kufikia umri wa miaka miwili mtoto huanza kukimbia, kupanda na kushuka katika vitu mbalimbali bila msaada. Pia, uwezo wa mtoto kutunza kumbukumbu na kuzungumza huongezeka. Hisia za kukasirika, furaha, huzuni na uoga ni baadhi ya tabia zinazoonekana katika hatua hii. Mtoto pia hujifunza kupenda na kuamini watu hasa wanaomhudumia na kumjali. Meno ya utotoni huanza kuota katika hatua hii.

 

(b) Utoto

Kipindi cha utoto huanzia kuanzia miaka miwili (2) hadi miaka kumina tatu (13). Katika kipindi hiki mtoto huongezeka kimo na uzito, hii huambatana na mabadiliko mengi katika miili yao. Katika hatua hii meno ya utotoni hutoka na meno ya kudumu huota. Mtoto hujenga uwezo mkubwa wa kupanda juu ya vitu mbalimbali, kuruka, kuendesha vitu mbalimbali, kukimbia, kula mwenyewe, kuchora na kupaka rangi. Mtoto hujifunza kutekeleza mahitaji yake ya kijamii kwa mfano kuvaa nguo, kula na kuoga mwenyewe. Katika kipindi hiki ukuzaji wa maarifa hutegemea sana msaada wa wazazi au walezi. Pia, mahusiano kati ya mtoto na wazazi au walezi ni muhimu sana katika kipindi hiki. Watoto wanatakiwa kupata mlo kamili, mazingira mazuri ya kucheza, huduma bora za kiafya, usafi wa mara kwa mara, mahali pazuri pa kulala na mavazi.

(c) Ukuaji wakati wa ujana

Hiki ni kipindi cha mpito kuelekea utu uzima. Kipindi hiki kinahusisha kubalehe kwa kijana. Balehe ni kipindi kinachotambulika kama kipindi cha mpito kutoka utoto kwenda utu uzima. Katika kipindi hiki, mabadiliko makubwa ya kiakili, kimaumbile, kimahusiano na kitabia hutokea. Kipindi hiki pia huchagizwa na vichocheo vya mwili yaani homoni zinazosababisha mabadiliko ya kimwili na kiakili. Kwa kawaida wavulana huingia katika kipindi cha balehe wanapofikia umri wa miaka 12 hadi 13 na wasichana huingia katika kipindi cha balehe kati ya umri wa miaka 11 hadi 12. Baadhi ya wavulana na wasichana huwahi au huchelewa kuliko muda wa wastani wa kuingia balehe. Hali hiyo ya kuwahi au kuchelewa hutegemea sababu za kijenetiki, lishe na mazingira.

 

Mabadiliko ya kimaumbile wakati wa balehe

Msichana na mvulana huonesha mabadiliko mbalimbali wakati wa balehe.

(a) Mabadiliko ya kimaumbile wakati wa balehe kwa msichana

Kwa upande wa msichana mabadiliko hayo humfanya msichana kuwa na mwonekano.

Mabadiliko ya kimaumbile kwa msichana wakati wa balehe hujumuisha:

(i) Kukua na kuongezeka kwa matiti.

(ii) Kuongezeka kwa utendaji kazi wa tezi za jasho.

(iii) Kuongezeka kwa ute katika uke.

(iv) Kukua kwa nywele za kwapani na sehemu zinazozunguka uke.

(v) Kuongezeka kwa kimo na uzito.

(vi) Sauti kubadilika na kuwa nyororo.

(vii) Kuota chunusi usoni.

(viii) Kupanuka kwa sehemu ya kiuno au nyonga.

(ix) Kupevuka kwa mayai na kuanza kupata hedhi au kuvunja ungo.

 

Mzunguko wa hedhi

Hedhi ni mchakato wa asili wa kibaiolojia wa utokaji wa damu iliyochanganyika na uteute kutoka kwenye ukuta wa uterasi kupitia uke. Hedhi ya mara ya kwanza ni moja ya ishara ya msingi ya kubalehe kwa msichana. Hedhi hutokana na kubomoka kwa utando na kuta za mji wa mimba, yaani uterasi. Kwa kawaida, hedhi hutokea mara moja kwa mwezi

kama sehemu ya mzunguko wake ambapo yai moja au zaidi hupevuka. Mzunguko wa hedhi ni kipindi kuanzia siku ya kwanza ya hedhi hadi siku moja kabla ya hedhi inayofuata. Kwa kawaida mzunguko wa hedhi ni siku 28 kama Kielelezo namba 6 kinavyoonesha. Hata hivyo, kuna wanawake wengine wana mzunguko wa kati ya siku 21 na 35.

Kielelezo: mzunguko wa hedhi wa siku 28

Kuanza kwa hedhi kunaashiria kubomoka kwa ukuta wa uterasi ambao ulikuwa umejengeka kwa ajili ya kupokea zaigoti endapo yai lingerutubishwa. Muda wa hedhi hutofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine. Kwa kawaida hedhi hudumu kati ya siku 3 hadi 5. Ingawa, baadhi ya wanawake wanaweza kuwa na hedhi fupi zaidi au ndefu hadi kufikia siku 7. Wakati wa hedhi vifaa maalumu vinavyoitwa pedi za kike au taulo za kike hutumika kufyonza damu inayokuja kupitia uke. Inashauriwa kutumia pedi za pamba. Pedi huvaliwa ndani ya chupi kwa kutumia vibandiko au vibawa maalumu. Inashauriwa kubadilisha pedi mara kwa mara, walau kila baada ya masaa matatu mpaka manne, ili kudumisha usafi na kuzuia matatizo yanayoweza kutokea kama vile harara au maambukizi.

 

Kasoro katika mzunguko wa hedhi

Wakati mwingine kasoro hutokea katika mzunguko wa hedhi. Miongoni mwa kasoro hizo ni hali ya kujisikia vibaya wakati wa mzunguko wa hedhi, kukosa hedhi, maumivu makali wakati wa hedhi na kutokwa na damu nyingi kwa muda mrefu. Kasoro hizi zinaweza kusababishwa na mabadiliko ya homoni, msongo wa mawazo au matatizo ya kiafya.

Kujisikia vibaya wakati wa hedhi: Kwa baadhi ya wanawake hedhi huambatana na kujisikia vibaya. Hii ni hali ambayo inaweza kumfanya mtu ashindwe kufanya kazi zake kwa ufanisi katika kipindi cha hedhi. Athari za hali hii zinaweza kuwa za saa chache na kwa wengine siku nyingi. Hali hii hutofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine. Hali hizo ni pamoja na sonona, hasira, mchafuko wa tumbo, kuumwa kichwa, kizunguzungu, mapigo ya moyo kwenda kasi, kukosa hamu ya kula na kujaa maji kwenye miguu, mikono na vidole. Ili kupunguza makali ya hali hii inashauriwa kufanya mazoezi walau mara 3 hadi 5 kwa wiki. Pia, kula mlo kamili ukijumuisha na matunda, kulala kwa muda wa kutosha na kupumzika.

Maumivu makali wakati wa hedhi: Baadhi ya wanawake hupata maumivu makali wakati wa hedhi. Maumivu haya yanaweza kutokea tangu msichana anapo balehe au huanza baadaye. Maumivu haya hutokea kutokana na kujifinya kwa kuta za uterasi kutokana na uwiano usio sahihi wa homoni mwilini. Sababu nyingine zinazoweza kusababisha maumivu wakati wa hedhi ni maambukizi ya magonjwa katika mlango wa kizazi. Vilevile, husababishwa na uvimbe katika tumbo la uzazi na maambukizi ya magonjwa katika mfumo wa uzazi. Matatizo haya yanaweza kumpata mwanamke yeyote. Hata hivyo, wanawake wenye uwezekano mkubwa zaidi wa kupata tatizo hili ni wale wanaovuta sigara, kunywa pombe, na wenye uzito mkubwa pamoja na wale wanaofikia balehe wakiwa na umri mdogo wa kabla ya miaka 11.

Kutokwa damu nyingi kuliko kawaida: Baadhi ya wanawake hupata tatizo la kutokwa na damu nyingi kuliko kawaida wakati wa hedhi. Wengine hupata hedhi siku nyingi kupita siku za kawaida za hedhi. Kiwango hiki huweza kusababishwa na damu kuto kuganda kwa muda mwafaka. Pia, kasoro katika mfumo wa homoni zinaweza kusababisha mwanamke kutokwa damu nyingi kuliko kawaida wakati wa hedhi.

 

(b) Mabadiliko ya kimaumbile wakati wa balehe kwa mvulana

Wakati wa balehe mvulana huwa  na baadhi ya mabadiliko kama ifuatavyo:

(i) Kukua kwa korodani na uume.

(ii) Kuongezeka kwa utendaji kazi wa tezi za jasho.

(iii) Kukua kwa nywele za kwapani na kuzunguka sehemu za siri, kifua, tumbo na ndevu kwa baadhi ya wavulana.

(iv) Kuongezeka kwa kimo na uzito.

(v) Sauti kubadilika kuwa nzito.

(vi) Kuota chunusi usoni kwa baadhi ya wavulana.

(vii) Kupata ndoto nyevu.

(viii) Kupanuka kwa misuli sehemu za kifuani na mikononi.

 

Mabadiliko ya kijamii wakati wa balehe

Katika kipindi cha balehe baadhi ya mabadiliko ya kijamii yanayotokea kwa wasichana na wavulana ni kama yafuatayo:

(a) Kuanza kujitambua: Katika kipindi cha balehe vijana wanaanza kujidadisi na kujitambua vizuri, kuwa ni wasichana au wavulana na kuanza kujenga uhusiano wenye hisia.

(b) Kutaka kutambuliwa: Vijana katika kipindi hiki huwa katika harakati ya kutaka kutambulika kwa nafasi zao katika jamii na dunia kwa ujumla. Harakati hizi zinaweza kuathiriwa na jinsia, kundirika, tamaduni na mategemeo ya familia.

(c) Kutaka kuwa huru: Katika kipindi hiki vijana huwa wanataka kuwa huru na kujiamulia mambo yao wenyewe bila kuingiliwa na wazazi au walezi. Hali hii mara nyingi husababisha migogoro kati ya vijana na wazazi au walezi wao. Wazazi au walezi wana wajibu wa kuwaongoza vijana wao, lakini vijana huona wana uhuru wa kuamua mambo yao. Vijana wana wajibu wa kutambua nafasi ya wazazi au walezi na kuwa na uhuru wenye mipaka.

(d) Kutaka kujifunza mambo mapya: Vijana wakifikia kipindi cha balehe, hupenda kujifunza mambo mbalimbali mapya na kujaribu vitu mbalimbali. Hali hii huwasababisha kuingia katika tabia hatarishi katika maisha. Katika kipindi hiki vijana hupenda kujifunza stadi mbalimbali kama kuendesha gari na pikipiki. Pia, baadhi ya vijana huanza kuvuta sigara au kutumia dawa za kulevya. Tabia hii husababisha kuanza kufanya ngono, hivyo kusababisha mimba zisizokusudiwa au maambukiz: ya virusi vya UKIMWI na magonjwa ya ngono.

 

Mabadiliko ya kiakili wakati wa balehe

Katika kipindi cha balehe wasichana na wavulana huwa na mabadiliko ya kiakili. Mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo:

(a) kutambaa mambo yanayowazunguka katika uhalisia wake.

(b) kujenga stadi za kutafuta matatizo magumu na yenye utata.

(c) kuelewa mawazo ya mtu mwengine.

(d) Kupuuza athari za beachi ya matendo wanayofanyafanya.

 

Mabadiliko ya kimahususi wakati wa balehe

Wakati wa balehe wasichana na wavulana huonesha mabadiliko katika uhusiano wao na jamii inayowazunguka. Mabadiliko hayo ni kama yafuatayo:

 

(a) Kupenda kukaa na marafiki kwa muda mrefu kuliko familia:

Katika kipindi hiki kijana huona marafiki zake ni wa muhimu zaidi kuliko wazazi, walezi au ndugu zake. Hushiki kwamba marafiki zake wanamweleza zaidi kwa kuwa mawazo yao yanadendana. Hivyo, huona ni vyema kukaa na vijana wenzake kuliko wazazi, walezi au ndugu zake.

(b) Kuwa na mitazamo tofauti na watu wazima:

Haii li inatokana na kupenda kujenga mitazamo yake mwenyewe na kuhoji kila anachokiona na kukisikia. Huthofu kuigana mambo yake arayo nae na hali. Kwa kawada mitazamo hii húsababisha migogoro kati ya kijana na wazazi, walezi au ndugu zake. Hali hiyo, migogoro hii haina halirafiki uhusiano kati ya kijana, mzazi, mlezi au ndugu kwani ni hali ya mipito tu.

 (c) Kupenda kushindana: Hiki ni kipindi ambacho vijana hupenda kushindana na kuigizanisha na wenziwa katika masuala mbalimbali. Wanapenda kuonekana kwao wao wanafanya vizuri katika kila jambo nyumbani na hata nje ya nyumbani. Hupenda kuonekana kama mfano wa kuiga.

 

Mabadiliko ya kihisia

Mabadiliko yanayotokea katika hisia za wasichana na wavulana katika kipindi hiki cha balehe ni kama yafuatayo:

(a) Kuonesha hisia kali na za ndani katika nyakati tofauti: Hisia za vijana katika kipindi hiki hubadilishana mara kwa mara. Jambo dogo linaweza kumharibisha, kumkushirisha au kumisimisha. Katika kipindi hiki mshoneno au mvutano anaeza kulia au kuwa na hasira kali kutokana na jambo dogo dogo. Hali hii ya kawada kwa vijana au hubadilishana na hali ya ubongo au wakijana kuwa machakato au kutaka kuonesha hisia katika hali ya utu uzima. Jambo hili linaweza kuongeza migogoro ya mara kwa mara katika familia na jami anaoishi endapo hawalimwelewa na kujaa naye taratibu.

(b) Kuonesha kujipendelea zaidi: Katika kipindi hiki kijana anaijali zaidi kuliko watu wengine. Anapenda kuonekana vyema vizuri kimaumbile na kimawazo. Pia, anaeza kujilingisha umbo lao na maumbo ya vijana wa kundirika moja au kundirika lingine. Hii ndiyo ‘shabubu’ vijana wengi huiga watu wanaowaza ni maafufu namna ya kuvaa, kunywa, kuonekana na hata kutembea.

 

Nja za kuhimili mabadiliko yanayotokea walafu wa balehe

Mabadiliko yanayotokea wakati wa balehe kwa mischana na mfululano hayepeki. Hata hivyo, kuna mbinu mbali mbali zinazoweza zikifuatwa ipasavyo zingazweza kupunguza au kuondoa changamoto zinazozambatana na mabadiliko hayo. Ili kupunguza athari zinazotokeza kutoka wakati wa balehe inashauriwa kufanya mambo yafuatayo:

Kufanya mazoezi:Wakati wa balehe kijana hukua haraka na kuongezeka uzito na hivyo kwa wa nguvu nyingi. Mazoezi yanasaidia mzunguko wa damu na hewa ya oksijeni na hivyo hufanya mwili kuchangamka na kuondoa msongo au mawazo na kujiskia furaha.

Kula chakula mizuri na kutosha na kula na kamili: Kulala usingizi kwa muda wa kutosha unahumu mwili kuwa mwil uunacuk. Usingizi wa kutosha husaidia kuondoa uchovu na kusawazisha viwango vya nishati. Lishe bora inayochukua vyakula vyenye virutubisho muhimu huchangia katika ukuaji wa afya ya mwili na akili.

Kuepuka matumizi ya pombe, tumbaku na vilevi vingine: Vilevi huathiri utendaji wa mfumo wa fahamu na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi. Kwa kuwa katika kipindi hiki kuna changamoto za kushindwa kufanya maamuzi mawili. Inashauriwa kuepuka kutumia vilevi na badala yake kufulia mtindo wa maisha afya bora. Pia, ni vyema kudumisha heshima kwa wengine ili kukuzia maadili mema.

Kushirikiana marafiki au ndugu katika changamoto wanazopitia: Changamoto marafiki au balehe humkusha kila kijana kwa hamna yake. Mara nyingine kijana hudhani kwa na yeye tu anaepukana na hali hiyo. Mawazo hayo huongeza mehemko, wasiwasi na kutojaliwa. Kushirikisha kijana katika changamoto wanazopitia, husaidia kupata ushauri sahihi kuhusu namna ya kukabiliana na changamoto wanazopitia.

Kuomba msaada kwa watu au kuamini: Wakati mwingine katika kipindi cha balehe, vijana hupta changamoto pa kushindwa kukabiliana nazo. Ni muhimu kuomba msaada kutoka kwa walezi, walimu, watu wengine wanaoona.

Kuzingatia usafi wa mwili: Usafi wa mwili ni muhimu katika kipindi cha balehe. Usafi huo ni kama kuoga, kufua nguo, kupiga pasi na kunywa nywele. Kwa wasichana ni muhimu kubadilisha kwa wakati taulo za kute wanazozivaa wakiwa na hedhi.

(d) Utu uzima

Hatua ya utu uzima ni kipindi ambacho ukuaji wa mwili hufikia kimo mo au huendelea kukua taratibu. Mwili wa binadamu hutumia nguvu zedi kudumisha afya ya mifumo yake kuiko kuongezeka kwa uzima. Kipindi hiki kinatokaeza umriza mika 18-65. Katika kipindi hiki cha utu uzima ukuaji unakuwa huweza mishwio na uwezo wa kazi, hua huwa umekamilika. Mtu umriza huweza kuijamini na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi na kuwaijika katika masuala mbalimbali za kimaisha, ufanayi wa mazoezi, mi kamili, mavazi na malazi safi.

(e) Uzee

Kipindi hiki cha uzee huanzia miaka 65 na kuendelea. Katika kipindi hiki mifumo ya mwili huzorota na mwili kudhoofika ukilinganisha na ujana. Uwezo wa nguvu za mwili hupungua, mvi hutokea na uwezo wa kushika hubunguka. Ngozi hujanibisha na uwezo wa kutunza kumbukumbu hupungua. Wazee hujaliwa mafunzo wa kuhusu usafi, ulaji wa mlo kamili, na ufanyaji wa mazoezi mepesi. Uangalizi wa afya kwa mara kwa mara ni muhimu ili kuweka afya zao vizuri.


 

SURA YA TATU: MFUMO WA UZAZI

Dhana ya mfumo wa uzazi wa binadamu.

Kuzaliana ni mchakato wa kibaolojia ambapo viumbehai hutengeneza uzao mpya. Kuzaliana huongeza idadi ya viumbe na kuhakikisha uwepo wa spishi. Kuzaliana huendelea kuwepo kuliko kizazi kinjia hadi kingine. Kuna aina mbili za kuzaliana, ambazo ni uzao wa nje na ujamiwa hadi uzao. Uzao wa nje ni wa kutokujamiiana (nafasi). Kuzaliana kwa nje ni ya kujamiiana kunahusisha wazazi wawili (wa kiume na kike) na kuungana kwa seli za uzazi zao ili kuumba ya yai la mwanamke ili kutengeneza uzao mpya. Kwa upande mwingine, kuzaliana bila ya kujamiiana kunahusisha mzazi mmoja tu na hutengeneza uzao mpya wananaofana kabisa na mzazi huyo. Binaadamu na viumbe veringine, kuzaliana huevezesha na mfumo wa uzao.

Mfumo wa uzazi ni mkusanyiko wa ogani za michakato inayohusika na uzalishaji wa viumbehai. Kwa binadamu, mfumo wa uzazi unaweza kugawanyika katika sehemu mbili wa kumbembe na wa kike ambapo kila mmoja una ogani maalumu zinazofanya ili kuwezesha uzazi. Uzazi kwa binadamu huwezekana baada ya kubaliana. Kifendo cha uzalishi kwa binadamu kinahusisha utengenezaji wa gameti. Gameti zime utengenezwa ndani ya korodani na gameti uke au yai hutengenezwa ndani ya ovari.

Mfumo wa uzazi unafadhiliwa na vichocho au homoni kama vile oestrogeni, projestroni, na testosteroni, ambazo zina jumla la kudhibiti ukubwa wa uzazi kwa uzazi, mzunguko wa hedi, uzalishaji wa gameti ya mwanamke. Mfumo huu ni muhimu kwa binadamu kwani husababisha ongezeko la idadi ya vyumbehai jamii. Hivyo, husaidia kuwepo kwa mwendoleo wa vizazi. Pia, huwezesha kurithisha sifa zao na kuchangia katika kuendelea kwa vinasaba kutoka kizazi kimoja hadi kingine.


 

Mfumo wa uzazi wa binadamu

Mfumo wa uzazi wa mwanaume.

Mfumo wa uzazi wa mwanaume una sehemu kuu mbili ambazo ni sehemu za nje na sehemu za ndani. Sehemu za nje zimeundwa na uume na korodani. Sehemu za ndani zimeundwa na mirija ya manii, urethra, kifuko cha manili, tezi dume na tezi za kopa. Kielelezo namba 1 kinaonesha shemu za ndani na za nje za mfumo wa uzazi wa mwanaume.

Kielelezo: mfumo wa uzazi wa mwanaume

 

 

 

 

 

 

 

Jedwali: sehemu za mfumo wa mwanaume na kazi zake

No

sehemu

maelezo

Kazi

1

korodani

Hupatikana ndani

ya mfuko wa ngozi.

Korodani huning'inia

nyuma ya uume. Kila

mwanaume ana jozi

ya korodani.

- Kutengeneza gameti ume

na kuzihifadhi

- Kuzalisha homoni ya

testosteroni, inayohusika

na mabadiliko ya maumbile

kama vile ukuaji wa ndevu,

sauti kuwa nzito, na misuli

yenye nguvu katika kipindi

cha balehe.

2

Mirija ya manii

Mrija uliojizungusha

unaonganisha

korodani na urethra.

Kuhifadhi na kusafirisha

mbegu za kiume (gameti

ume) kutoka kwenye

korodani hadi kwenye

urethira.

3

uume

Ni mrija mwembamba

unaopatikana ndani

ya uume na hupita

kutoka kwenye

kibofu cha mkojo

hadi kwenye ncha ya

uume.

- Kusafirisha mbegu za kiume zilizochanganyika na majimaji ya manii kwenda kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke.

- Kusafirisha mkojo kutoka kwenye kibofu cha mkojo hadi nje ya mwili.

4

urethira

Ni mrija mwembamba

unaopatikana ndani

ya uume na hupita

kutoka kwenye

kibofu cha mkojo

hadi kwenye ncha ya

uume.

- Kusafirisha mbegu za

kiume zilizochanganyika na

majimaji ya manii kwenda

kwenye mfumo wa uzazi

wa mwanamke.

- Kusafirisha mkojo kutoka

kwenye kibofu cha mkojo

hadi nje ya mwili.

5

Kifuko cha manii

Ni jozi ya ogani

ndogo za mfumo wa

uzazi wa mwanaume

zilizopo karibu na

tezi dume, nyuma ya

kibofu cha mkojo.

Kutengeneza na kutoa

majimaji yenye virutubisho

ambavyo hutoa nishati kwa

mbegu za kiume ili ziweze

kuogelea kuelekea yai la

mwanamke.

6

Tezi dume

Ni ogani

inayopatikana chini

ya kibofu cha mkojo,

ikizunguka sehemu

ya juu ya urethira.

Kutoa majimaji mazito yenye

utelezi ambayo husaidia

kulinda na kujongea kwa

kuogelea tezi kopakwa mbegu za

kiume.

7

Tezi kopa

Ni jozi ya ogani

zinazopatikana chini ya

tezi dume

Kutoa majimaji yanayosaidia

kupunguza asidi katika

urethira, ili kuandaa upitishaji

wa mbegu za kiume.

 

 

Mfumo wa uzazi wa mwanamke

Mfumo wa uzazi wa mwanamke ni mfumo unaohusika na uzalishaji wa mayai au gameti uke, utoaji wa homoni, na kutoa mazingira ya kutungwa kwa mimba na ukuaji wa mtoto. Mfumo huu umeundwa na sehemu kuu nne, ambazo ni ovari, mirija ya falopio, uterasi na uke.  Mfumo wa uzazi wa mwanamke unadhibitiwa na homoni za estrogeni and projesteroni, zinazosaidia mzunguko wa hedhi, mimba na mchakato wa kuzaa.

Kielelezo: mfumo wa uzazi wa mwanamke

Na

Sehemu

Maelezo

Kazi

1

Ovari

Ni jozi ya tezi za

uzazi zilizopo upande

wa kulia na kushoto

Wwa uterasi.

- Kutengeneza na kuhifadhi

gameti uke au ova.

 

- Kutoa homoni muhimu

kama oestrojeni na

projesteroni, ambazo

husaidia kudhibiti

mzunguko wa hedhi,

ukuaji wa ogani za uzazi

na kuwezesha ujauzito.

Homoni hizo pia zinahusika

na mabadiliko mbalimbali

kwa msichana wakati wa

balehe.

2

Mirija ya falopio

Ni mirija miwili

inayopatikana

upande wa kushoto

na kulia mwa mji

wa mimba (uterasi).

Mirija hii huunganisha

ovari na uterasi.

- Kusafirisha yai kutoka

kwenye ovari hadi mji wa

mimba. Pia, husaidia katika

kuvuta na kuelekeza yai

kuelekea mji wa mimba.

 

- Ni sehemu ambayo

urutubishaji wa yai

hufanyika.

3

Uterasi (mji wa mimba)

Ni mfuko wenye kuta

za misuli minene.

Wakati wa mimba,

kijusi hukua na

kukomaa ndani ya

uterasi hadi wakati

wa kujifungua.

- Kutoa mazingira ya kukua

kwa kijusi wakati wa

ujauzito.

- Kutengeneza mji wa mimba

4

Mlango wa kizazi

Ni sehemu ya

chini ya mji wa

mimba (uterasi)

inayounganisha

uterasi na uke.

- Kudhibiti na kuruhusu

mtiririko wa damu wakati

wa hedhi.

 

- kupokea mbegu za kiume

na kutoa njia ya kupita

mtoto wakati wa kujifungua.

5

Uke

Ni sehemu

inayopatikana kati

ya shingo ya kizazi

nasehemu za nje za

mwili.

- Kupokea mbegu za kiume.

- Kupitisha mtoto wakati wa

kujifungua.

- Kutoa njia ya damu wakati

wa hedhi.

- Hulinda viungo vya uzazi

dhidi ya maambukizi, kwani

hutoa mazingira ya asidi

ambayo yanazuia bakteria

hatari.

 

Kasoro katika mfumo wa uzazi

Kasoro katika mfumo wa uzazi ni hali au changamoto zinazoweza kuathiri uwezo wa mfumo wa uzazi wa kike au wa kiume kufanya kazi ipasavyo. Kasoro hizi zinaweza kuwa za kimaumbile au za kiafya. Kasoro hizi zinaweza kuwa za kurithi, mitindo mibaya ya maisha, lishe duni, magonjwa sugu au athari za kimazingira kama vile kemikali na mionzi hatari. Aidha, uchunguzi wa mara kwa mara na matibabu ya mapema ni muhimu ili kuzuia au kurekebisha matatizo na kasoro katika mfumo wa

uzazi wa mwanaume na mwanawake.

 

Kasoro katika mfumo wa uzazi wa mwanaume

Kasoro katika mfumo wa uzazi wa mwanaume ni changamoto zinazoweza kuathiri utendaji wa kawaida wa mfumo wa uzazi. Baadhi ya kasoro hizo ni kama ifuatavyo:

 

Ugumba

Hii ni hali ya mwanaume kushindwa kurutubisha yai la kike, na hivyo kushindwa kutungisha mimba. Ugumba kwa mwanaume husababishwa na mambo mbalimbali ikiwemo kutoa mbegu chache, hivyo kupunguza uwezekano wa kulifikia na kurutubisha yai. Pia, kuwa na mbegu dhaifu zisizo na uwezo wa kuogelea kuiifikia yai. Kuzalisha mbegu zenye upungufu kwa mfano mbegu zilizokosa mkia, kuwa na mikia miwili, kukosa kichwa au kuwa na umbo lisilo la kawaida.

Vilevile, korodani zinaweza kushindwa kutengeneza mbegu za kiume kutokana na magonjwa, lishe duni au upungufu wa homoni. Sababu nyingine ya ugumba ni mirja ya mani kuziba kutokana na magonjWaya ngono kama vile kisonono na kaswende.

 

Matatizo ya tezi dume

Hii i hali inayohusiana na uharibifu au kupanuka kwa tezi dume. Kasoro hizi zinaweza kuwa na madhara kwenye mfimo wa mkojo na uzazi. Kupanuka kwa tezi dume hutokana na maambukizi ya magonjwa au saratani. Tatizo hii hupelekea kuziba kwayUrethira fia kusababisha kukojoa kwa shida.

 

 

 

Kasoro katika mfumo wa uzazi wa mwanamke

Kasoro katika mfumo wa uzazi wa muanamke fii changamoto zinazoweza kuathiri utendaji wa kawaida wa mfumo wa uzazi. Baadhi ya kasoro hizo ni kama ifuatavyo:

 

Ugumba

Ni hali ya mwanamke Kushindwa kupata mimba kwa sababu mbalimbali. Ugumba husababishwa na'mambo mbalimbali ikiwemo mayai kushindwa kupevuka. Hali hii hutokana na matatizo ya utoaji wa homoni za oestrojeni au projesterofi.

Aidha, ugumba,unaweza kusababishwa na maambukizi ya magonjwa ya ngono kama kisonono, kaswende na pangusa. Magonjwa haya husababisha kuziba kwa mirja ya kupitisha mayai ili yarutubishwe. Magonjwa haya yanaweza kuifanya mirija iwe myembamba au iwe na makovu hivyo kuzuia yai lisiweze kupita.

 

Kasoro katika shingo ya mlango wa kizazi

Shingo ya miango wa kizazi inaweza kupata madhara kutokana na matatizo ya uzazi au maambukizi katika shingo ya miango wa kizazi. Hali hii inaweza kusababisha shingo ya kizazi kuwa na kasoro.

 

Kasoro za hedhi

Hizi ni kasoro zinazotokana na muda, kiwango cha damu inayotoka au kujisikia vibaya wakati wa hedhi. Moja ya kasoro ni kukoma au kutopata hedhi kwa mwanamke asiye na ujauzito kwa muda fulani. Kasoro nyingine ni pamoja na kupata maumivu makali wakati wa hedhi kutokana na kukaza kwa misuli ya uterasi. Pia, baadhi ya wanawake hupata shida ya kutokwa na damu kwa muda mrefu kuliko kawaida wakati wa hedhi. Kasoro hizi husababishwa na matatizo ya uzalishwaji wa homoni, hasa upungufu wa utolewaji wa homoni ya oestrojeni, matatizo ya kijenetiki, magonjwa sugu, na sonona. Kasoro hizi zinaweza kutibiwa na hivyo ni muhimu kupata ushauri wa kitabibu.

Utunzaji wa mfumo wa uzazi

Mfumo wa uzazi ni muhimu kwa ustawi wa binadamu. Hivyo ni muhimu kutunza mifumo ya uzazi ili kuepukana na madhara yanayoweza kutokea na kuharibu au kupunguza ufanisi wake. Madhara hayo ni kama vile maambukizi katika sehemu za uzazi yanayopelekea magonjwa. Mfano wa magonjwa ya mifumo ya uzazi ni kama vile magonjwa ya zinaa, maambukizi ya fangasi, bakteria na vijidudu vingine kwenye via vya uzazi. Ili kutunza mifumo ya uzazi tunapaswa kufanya yafuatayo:

 

Kuzingatia usafi

Ni muhimu kuzingatia usafi wa mwili kwa kuoga kwa maji safi na sabuni kila siku. Pia, ni muhimu kusafisha sehemu za siri kila mara unapotoka kujisaidia kwa kutumia maji safi. Vilevile, kutumia vyoo visafi na kuzingatia usafi chooni ni muhimu katika kulinda mifumo ya uzazi. Kuvaa nguo za ndani zilizo kavu na safi kila siku pamoja na kuepuka kuchangia nguo za ndani na mtu mwingine ili kuepuka maambukizi.

Kuzingatia lishe bora na mazoezi

Kupata lishe bora yenye virutubisho vinavyotakiwa katika uwiano sahihi na kunywa maji ya kutosha kunasaidia kutunza mifumo ya uzazi. Pia, kufanya mazoezi mara kwa mara kunasaidia kuimarisha mwili na mifumo yake. Mazoezi yanasadia pia kuepuka uzito uliopitiliza ambao huweza kuathiri mwili na mfumo wa uzazi.

Kuepuka tabia hatarishi

Baadhi ya tabia ni hatarishi kwa afya ya mwili wa binadamu. Utumiaji wa pombe, sigara na vilevi vingine huzorotesha afya ya mwili na mifumo ya uzazi pia. Ni vema kuepuka tabia hizi ili kuwa na mfumo wa uzazi ulio na afya.


 

SURA YA NNE: USUMAKU

Dhana ya usumaku

Usumaku ni uwezo wa sumaku kuvuta au kusukuma vitu. Sumaku hutumia uwezo huu kuvuta vitu vyenye asili ya chuma. Kwa hivyo, sumaku ni kifaa ambacho kina uwezo wa kuvuta vitu vyenye asili ya chuma. Kila sumaku ina ncha mbili. Ncha hizo ni ncha ya Kaskazini (KAS) na Kusini (KUS). Sumaku huzalisha uga wa sumaku. Uga wa sumaku ni eneo linazunguka sumaku ambalo kani ya sumaku huhisiwa. Kani ya sumaku ndiyo inayosababisha vitu kuvutwa au kusukumwa na sumaku. Kwa hiyo, kani ya sumaku kuvuta au kusukuma husababishwa na usumaku. Pia, kani ya sumaku huwakilishwa na mistari ya kufikirika inayoitwa mistari ya kani ya sumaku ambayo huonekana unaposambaza unga wa chuma kuzunguka sumaku mche mstatili. Unga wa chuma hujipanga kwa muundo maalum na kuunda mistari.

 

Maumbo ya sumaku

Sumaku inaweza kuonekana katika maumbo mbalimbali kulingana na matumizi yake. Mifano ya maumbo ya sumaku ni kama vile sumaku mche mstatili, sumaku kwatofarasi, sumaku U, sumaku duara na sumaku mche duara. Kila umbo huathiri jinsi sumaku inavyounda eneo la usumaku. Pia, umbo la sumaku huathiri matumizi

Yake.

Kielelezo: maumbo ya sumaku

Sifa za sumaku

Sumaku zina sifa mbalimbali muhimu ambazo huelezea tabia zake. Baadhi ya sifa hizo ni:

(a) Sumaku huvuta vitu vyenye asili ya chuma.

(b) Kani ya sumaku ni kubwa kwenye ncha za sumaku.

(c) Sumaku mbili zikikaribiana, ncha zinazofanana hukwepana na ncha zisizofanana huvutana.

Umbo la sumaku huathiri uwezo wa sumaku kuvuta vitu. Pia, ncha za sumaku zina kani kubwa zaidi ya kuvuta vitu kuliko sehemu zingine za sumaku, ambazo huwa zina kani ndogo ya kuvuta vitu.

 

Kanuni ya usumaku

Kanuni ya msingi ya usumaku inasema "Ncha za sumaku zinazofanana hukwepana na ncha zisizofanana huvutana".

Unaposukuma ncha mbili za kaskazini za sumaku kwa kuelekea, kani ya sumaku husukuma ncha hizo zisigusane. Hii ni kwa sababu nguvu za sumaku zinakwepana. Kwa upande mwingine, ncha ya kaskazini ya sumaku moja huvuta ncha ya kusini ya sumaku nyingine. Kazi hii inadhihirisha Kanuni ya usumaku.

 

Matumizi ya sumaku

Sumaku hutumika sehemu mbalimbali kama vile nyumbani, shuleni, hospitalini na viwandani. Yafuatayo ni baadhi ya matumizi ya sumaku. Kunyanyua vitu vizito Sumaku hutumika kuinua vitu vilivyo na asili ya chuma. Vitu hivyo vinaweza kuhamishwa kutoka sehemu moja hadi sehemu nyingine. Bandarini, sumaku pia hutumika katika upakiaji na upakuaji wa mizigo yenye asili ya chuma.


 

Kielelezo: sumaku ikiwa imenasa na kunyanyua mzigo

Matengenezo ya vifaa vya kielektroniki

Fundi simu, redio na kompyuta hutumia bisibisi na zana nyingine zenye sumaku kunasa skrubu ndogo za kufungia simu, redio au kompyuta. Kielelezo namba 9 kinaonyesha skrubu iliyonaswa na bisibisi yenye sumaku.

Kielelezo: bisisbisi yenye sumaku ikiwa imenasa skrubu

Kutengeneza kengele ya umeme

Sumaku hutumika kutengeneza kengele za umeme. Unapobonyeza kengele mkondo wa umeme huzalisha kani ya usumaku. Hivyo, kani ya usumaku husababisha kugongwa kwa kengele na kutoa mlio.

 

Kuonesha uelekeo

Dira ni kifaa chenye sumaku ambacho huonesha mwelekeo wa upande wa kaskazini na kusini wa dunia. Dira hutumika kuongoza watu kutambua pande kuu za dunia. Vilevile, hutumika kumwongoza nahodha wa meli na rubani wa ndege kwenda mwelekeo sahihi.

Kielelezo: Dira

Kuzalisha umeme

Sumaku hutumika kuzalisha umeme. Dainamo ya baiskeli ina sumaku ambayo imezungukwa na koili.  Gurudumu la baiskeli linapozunguka husababisha sumaku pia kuzunguka. Mzunguko wa sumaku huzalisha umeme kwenye koili. Umeme huo husafirishwa kwa waya kwenda kwenye taa na kusababisha taa hiyo kuwaka. Magurudumuya baiskeli yanapozunguka kwa kasi, umeme unaozalishwa huongezeka na taa huangaza zaidi. Magurudumu ya baiskeli yanapozunguka polepole,umeme hupungua na mwanga wa taa huwa hafifu.

Kielelezo: sumaku kwenye dainamo ya baiskeli

 

Kutenganisha vitu

Sumaku hutumika kutenganisha vitu vyenye asili ya chuma na visivyo na asili ya chuma. Mbinu hii hutumika katika viwanda vya vyakula, kutenganisha chembechembe za chuma kutoka kwenye bidhaa za chakula. Hii husaidia kuhakikisha usalama na kuzuia uchafuzi wa chakula.

Kielelezo: sumaku ikitengamnisha chembechembe za chuma kutoka kwenye unga

Sumaku hutumika pia katika vifaa mbalimbali vya kielektroniki na kiteknolojia. Baadhi ya vitu hivyo ni friji, redio, simu, kompyuta, jenereta, kadi za benki, vinasa sauti na vipaza sauti.


 

Utunzaji wa sumaku

Sumaku hupoteza kani pale ambapo ncha zake zitavutana na kuvurugampangilio wa chembechembe zilizo ndani ya sumaku. Sumaku hutunza kani yake kwa muda mrefu ikiwa tutazingatia yafuatayo:

(a) Kuweka sumaku mahali ambapo hazitachangamana na vitu vyenye asili ya chuma.

(b) Hakikisha kuwa ncha za sumaku zinazofanana hazielekeani.

(c) Kutoichoma moto sumaku.

(d) Kutoweka sumaku karibu na vitu vyenye usumaku mkubwa zaidi au umeme.

(e) Kutoponda au kugongagonga sumaku.


 

SURA YA TANO: USIMBIKAJI KATIKA KOMPYUTA

Muundo wa kudhibiti mlolongo

Katika muundo wa kudhibiti mlolongo, maelekezo ya programu hufanyika

kwa mpangilio maalumu, hatua moja baada ya nyingine. Hii inamaanisha

kuwa, maelekezo ya hatua ya kwanza hufanyika kwanza, kisha ya pili,

hadi ya mwisho.

Mfano mzuri wa kazi ambayo hufanyika kwa hatua ni uzalishaji wa mazao

shambani. Katika kupanda mazao shambani hatua zake ni:

1. Kuandaa shamba;

2. Kupanda mbegu;

3. Kupalilia; na

4. Kuvuna.

Zingatia kuwa, hatua hizi ni lazima zifuatwe kwa mpangilio huo ili kukamilisha kazi. Kwa mfano, huwezi kupanda mbegu kabla ya kuandaa shamba, kwa sababu mbegu hazitaota.

Hii dhana ya kufanya kazi kwa kufuata mlolongo hutumika pia kwenye programu za kompyuta. Kwa mfano, katika programu ya Scratch, tunatumia muundo wa kudhibiti mlolongo kwa kupanga bloku za maelekezo kutoka juu kwenda chini. Kompyuta itafuata maelekezo hayo katika mlolongo huo.

 

Vibadilika na opereta

Programu nyingi za kompyuta tunazotumia kila siku hufanya hesabu mbalimbali. Mfano, programu za kompyuta zinatumika benki na maduka makubwa kufanya hesabu zinazohusisha fedha na bidhaa. Fikiria umetembelea duka kubwa, ukanunua kalamu 3 kwa shilingi 300/= kila moja, rula moja kwa shilingi 500/= na pipi 2 kwa shilingi 100/= kila moja. Ukilipa kwa noti ya shilingi 2000/=, programu ya duka itahesabu jumla ya fedha unayotakiwa kulipa (yaani shilingi 1600/=) na pesa za kukurudishia kama chenji (yaani shilingi 400/=). Muhtasari wa taarifa za mfano huu

zimeoneshwa kwenye Jedwali lifuatalo.

 

Jedwali: Orodha ya manunuzi

Aina ya bidhaa

idadi

Bei ya kila bdhaa (shilingi)

Jumla ndogo (shilingi)

Kalamu

3

300/=

900/=

Rula

1

500/=

500/=

Pipi

2

100/=

200/=

Jumla

 

 

1600/=

 

Katika mfano huu, kila bidhaa ina idadi na bei. Ili programu ya kompyuta iweze kufanya hesabu hizi, inahitaji njia ya kuwakilisha vipimo hivyo (idadi

na bei). Njia hiyo ni kutumia vibadilika. Programu ya kompyuta inaweza kuwa na idadi yoyote ya vibadilika. Kila kibadilika kinatambulika kwa jina na kinaweza kuwa na kiasi tofautitofauti pindi programu inapoanzishwa na kuendelea kufanya kazi. Mifano ya vibadilika tunavyoweza kuviunda kutoka katika mfano huu ni IdadiYaKalamu (thamani = 3), BeiYaKalamu (thamani = 300) na BeiYaRula (thamani = 500). Inashauriwa unapopendekeza jina la kibadilika, pendekezajina litakalo kukumbusha kipimo kinachowakilishwa. Programu ya Scratch inaruhusu kuunda na kutumia vibadilika. Kabla ya kutumia kibadilika, unatakiwa ukiunde. Umalizapo matumizi ya kibadilika, unaweza kukifuta.

Kibadilika kikishaunndwa kinaweza kutumika sehemu mbalimbali kwenyeprogramu. Rejea mfano wa kutumia programu za kompyuta kwenye maduka makubwa, vibadilika vinaweza kutumika kutafuta jumla ndogo ya kila bidhaa, jumla kuu ya bidhaa zote pamoja na chenji utakayopokea. Mfano, kutafuta jumla ndogo ya kalamu, hesabu inaweza kuwakilishwa kama BeiYaKalamu * IdadiYaKalamu. BeiYakalamu na IdadiYakalamu vinawakilisha bei ya kila kalamu (ambayo ni shilingi 300) na idadi ya kalamu (ambayo ni 3) mtawalia.

Zingatia kwamba katika mahesabu, operata ya * imetumika kuwakilisha kuzidisha badala ya alama x inayotumika katika hisabati. Opereta nyingine unazoweza kutumia ni: kujumlisha (+), kutoa (-), kugawanya (/), na mabaki (%).

Mbali na opereta za sayansi ya namba, programu pia hutumia opereta za kulinganisha kama vile: ndogo kuliko (<), kubwa kuliko (>) na sawa na (=). Pia kuna opereta za kimantiki ikiwa ni pamoja na: na, au na si.

 Kazi za kufanya zifuatazo zinaonesha namna ya kutumia vibadilika na opereta katika kufanya hesabu.

 

Muundo wa kudhibiti marudio

Baadhi ya kazi zinahitaji kitendo fulani kurudiwa mara kadhaa kabla ya kupata matokeo ya mwisho. Katika usimbaji hili linajulikana kama marudio au vitanzi. Rejea kazi zifuatazo kwenye mchezo:

(a) Kusogeza kihusika hatua kumi kwenda kulia.

(b) Kusogeza kihusika kwenda kulia mpaka kiguse ukingo.

(c) Kuchezesha sauti wakati mchezo ukiendelea.

Kazi zote hizi zinahitaji kitendo kurudiwa mara kadhaa kabla ya kupata matokeo ya mwisho. Kazi ya kwanza inahitaji kusogeza kihusika hatua kumi kwenda kulia, utarudia kusogeza kihusika hatua moja baada ya nyingine hadi zifike kumi. Kwa kazi ya pili, unahitaji kusogeza kihusika kwenda kulia mpaka kiguse ukingo. Kwa kazi ya tatu, unahitaji kuchezesha sauti wakati mchezo ukiendelea, sauti inapaswa kurudiwa bila kumalizika mpaka mwisho. Kazi ya kwanza na ya pili kitendo kinachojirudia ni nenda hatua moja kulia na ya tatu kitendo kinachojirudia ni kucheza sauti.

Utabaini kuwa, kwenye mfano wa kwanza, kitendo kinarudiwa kwa idadi maalum (mara kumi). Katika mfano wa pili, kitendo kinarudiwa mpaka jambo fulani litokee (kihusika kiguse ukingo). Kwenye mfano wa tatu, kitendo kinarudiwa bila kikomo hadi mchezo uishe.

Hii inamaanisha kuwa kuna aina tatu za kurudiwa kwa kazi kwenye programu, ambazo ni rudia ( ), rudia hadi ( ) na milele. Kwa kitanzi cha rudia ( ), thamani iliyo ndani ya mabano inaonyesha ni mara ngapi kitendo kitajirudia. Kwa kitanzi cha rudia hadi ( ), thamani ndani ya mabano inaonyesha sharti litakalosababisha kitanzi kisimame. Kitanzi cha milele kitaendelea kutekelezwa bila kikomo hadi utakaposimamisha mwenyewe au kutumia kizuizi cha komesha. Katika Scratch, vitanzi hivi vinapatikana kwenye bloku za Kidhibiti.

Kielelezo: aina za vitanzi katika scratch

 

Muundo wa kudhibiti maamuzi

Baadhi ya kazi zinahitaji programu kuchagua kati ya vitendo tofauti kulingana na sharti fulani. Katika usimbaji, hili hujulikana kama uamuzi au uchaguzi. Rejea kazi zifuatazo katika mchezo.

(a) Ikiwa kihusika kitagusa ukingo wa jukwaa, badilisha rangi yake.

(b) Ikiwa namba ni shufwa, sema Namba ni shufwa, la sivyo sema Namba ni witiri.

Kazi hizi zote zinahitaji programu kufanya maamuzi. Katika kazi ya kwanza, programu ina chaguo moja, kubadilisha rangi ikiwa ukingo utaguswa. Katika kazi ya pili, programu ina chaguzi mbili, kusema Namba ni shufwa au Namba ni witiri. Ili kufanya maamuzi rahisi katika Scratch, bloku ya ikiwa () basi inatumika. Vivyo hivyo, ili kuchagua kati ya chaguzi mbili, bloku ya ikiwa () basi isivyo inatumika.

Kielelezo: Bloku za ikiwa () basi na ikiwa ( )basi () isivyo lli programu iweze kufanya uamuzi, inahitaji taarifa ya awali. Taarifa hii inajulikana kama sharti-kwa ajili ya muundo wa udhibiti wa maamuzi, na huwekwa kwenye umbo la pembe sita lililopo juu ya bloku la maamuzi.

 

Kuchora maumbo kwenye Scratch

Maumbo ni miongoni mwa vitu vinavyotumika kuunda michezo rahis inayoshirikisha. Ili kuchora umbo katika Scratch, unapaswa kuongeza kiendelezi cha Kalamu. Kuongeza kiendelezi cha Kalamu, fuata hatua zifuatazo:

1. Bofya ikoni ya Ongeza kiendelezi iliypo kona ya chini kushoto. Angalia Kielelezo (a).

2. Bofya kiendelezi cha Kalamu ili kuongeza kwenye jalada lako la programu. Angalia Kielelezo (b).

Kielelezo: kuendeleza kiendelezi cha kalamu


Mifano ya bloku ya kiendelzi cha kalamu ni:

Post a Comment

Visit Website
Visit Website